BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 525
- 1,257
Nafahamu kwamba suala la uumini au dini ni pana, kuna baadhi ya mambo kulingana na Katiba yetu na miongozo mbalimbali Serikali inaweza kufungwa mikono kuyaingilia moja kwa moja, lakini kuna uwezekano kwenye baadhi ya vitu Serikali haifungwi mikono kuviingilia hususani suala la usalama wa Waumini.
Kati ya suala ambalo limekuwa likishangaza hasa kutokana na kutosikia baadhi ya Viongozi wa nyumba husika za Ibada au Serikali wakikemea ni vitendo vya baadhi ya waumini kunywa mafuta ambayo yanafahamika kama 'mafuta ya upako' na majina mengine ya aina hiyo kinyume na ilivyozoeleka siku za nyuma.
Kwa mara kadhaa nimeshuhudia mubashara suala hilo likifanyika katika makutano mbalimbali ya Ibada huku pia nikiwasikia baadhi Viongozi wanaoratibu huduma hizo wakiwaelekeza waumini kwamba wanaweza kutumia mafuta hayo kwa njia mbalimbali ikiwemo kuyanywa.
Licha ya kushuhudia lakini pia kupitia Vyombo vya Habari (Televisheni, Redio, Mitandao ya Kijamii) ni mara nyingi nimeona na kusikia baadhi ya Watu wakitoa ushuhuda mbele waandesha Ibada, kwamba walikunywa mafuta wakatendewa miujiza. Watu wanasema hayo wala hakuna ambaye anayakemea badala yake waamini wanaambiwa wapige makofi.
Bila kujiingiza kwenye mjadala wa uponyaji au mafuta hayo kuwezesha miujiza kutendeka kama inavyodaiwa, wasiwasi wangu na hoja yangu najiuliza je, mafuta hayo ni salama kwa matumizi ya binadamu akiyanywa?
Imekuwa ikisikia baadhi ya Wataalamu wa Afya wakizungumzia athari za mafuta mengi kwenye mwili wa binadamu, najiuliza au mafuta hayo yamewekewa kinga maalumu ambayo inayatofautisha na mafuta mengine ambayo yamekuwa yakielezwa juu ya athari zake pale yanapozidi kwenye mwili wa binadamu.
Kwa kuwa jambo hili linagusa ustawi wa Wananchi, wito wangu nauelekeza kwa mamlaka za Kiserikali kufuatilia kwa kina na kuchukua hatua za haraka ili kuweka afya za Wananchi katika usalama na kuwaondoa wengine hofu kwa sababu kwa siku za hivi karibuni kumeibuka wimbi la Watu kutumia mafuta hayo.