The Father of All
JF-Expert Member
- Feb 26, 2012
- 11,099
- 13,709
Huwa nasoma na kuchanganyikiwa. Watu wamegeuka mazwazwa hadi kushabikia uovu na uuaji! Japo siyo shabiki wa siasa za mashariki ya kati kwa sababu ni mambo yao, kinachoendelea Palestina kinaudhi na kuigeuza dunia sehemu ya wanyama.
Mataifa yanayojifanya kupigania na kulinda haki za binadamu yako kimya yakitoa misaada kwa jambazi Netanyahu. Hata wachovu wasio na nguvu, badala ya kulaani unyama huu, nao ajabu, wanashangilia. Leo Palestina. Nani anajua ya kesho?
Unyama ni unyama.
Ukatili ni ukatili.
Ushenzi ni ushenzi.
Hata akifanyiwa adui yako, ilmradi ni mja kama wewe, sioni haja ya kushabikia na kufurahia. Shame on you all akiwamo Trump na Musk.