Mr pianoman
JF-Expert Member
- May 22, 2019
- 2,595
- 6,264
Nakuuliza wewe Rais wangu Magufuli umekuwa madarakani miaka yote mitano inamaana ulikuwa huoni umuhimu wa kuvifanya hivyo vitu mpaka leo hii kipindi cha kampeni ndio utoe amri vifanyike?
Umetoa amri ya kuajiri walimu, Umetoa amri ya kujenga barabara huko kanda ya ziwa na nyingine nyingi tu sasa muda wote huo ulikuwa wapi hukufanya hivyo mpaka leo kwenye kampeni?
Kwenye suala la ajira kila mwaka bunge lilikuwa linapitisha bajeti ya ajira mpya ulikuwa hulijui hilo kweli mheshimiwa? Basi toa zile ajira zote zaidi ya elfu 46 zilizo pitishwa na bunge mwaka huu ili tuone kweli unatekeleza kweli au ndio unatuchora wapiga kura wako?
Hivi hujui na Watanzania nao wanakuchora tu kama wewe unavyo wachora hapo jukwaani kwa kuwahadaa na ajira za walimu na barabara? Watangulizi wako hayo mambo walikuwa wanayafanya kabla ya uchaguzi ndio maana watanzania waliwapa miaka 10 ya uongozi bila ubishi.
Magufuli hukupaswa leo kufanya hivi unavyofanya leo jukwaani kwani serikali yako imekuwa ikijinasibu kila kukicha imefanya makubwa. Ni kweli mmefanya makubwa ila makubwa bila kugusa maisha ya mtu binafsi na kudili na vitu hizo ni sifa za kijinga na ndicho kinacho wakosti leo kwenye kampeni.
Leo hii mtu aliye kuwa kwa mabeberu kwa zaidi ya miaka mitatu anaonekana wa maana zaidi kwa wananchi kuliko wewe unae jiita mzalendo ambaye kwa miaka mitano yote ulikuwa humu humu ndani ukipiga kazi! Kuna tatizo sehemu.