Uchaguzi 2020 Hivi Magufuli, hivyo vitu unavyoamuru vifanyike kipindi hiki cha kampeni ulikuwa wapi siku zote kufanya hivyo?

Uchaguzi 2020 Hivi Magufuli, hivyo vitu unavyoamuru vifanyike kipindi hiki cha kampeni ulikuwa wapi siku zote kufanya hivyo?

Huyu mzee siasa hajui ye ni mnyapala tu tuombe Mungu asitawale milele kama anavyopanga.
 
Kwa sasa hivi kwa ushauri wako kila kitu kisimame hadi uchaguzi au?
Elewa mantiki ya mtoa post, fungu la barabara ya Nyehunge limepitushwa na bunge gani, miaka mitano hujatoa ajira unakuja kuajiri kipindi hiki, hiyo ni rushwa tu.
 
Hahaha .ajira no kada nyigi haha ajiri .hata hao walimu hajawamaliza mtaani.lingine ni .jee nyongeza ya mishahara kwa watumishi Napo afanye.kuanzia 2016 aweke nyongeza ya Kila mwaka Hadi mwaka huuu.atangulie kwa kuwaomba radhi watumishi.
 
Umeanza maelezo vizuri kwa kumtaja Magufuli ni rais wako, cjajua umevurugwa nn kuanza kumponda rais wako! Kwa namna ulivyoanza maelezo, ulikuwa sahihi kikatiba, cjui imekuwaje ukatoka nje ya katiba!
 
Umeanza maelezo vizuri kwa kumtaja Magufuli ni rais wako, cjajua umevurugwa nn kuanza kumponda rais wako! Kwa namna ulivyoanza maelezo, ulikuwa sahihi kikatiba, cjui imekuwaje ukatoka nje ya katiba!
Simpondi ila namshauri afu nipo kwenye katiba bado maana ni haki yangu kujieleza na kuhoji.
 
JPM ndio rais aliyeko ambaye yuko usimlinganishe na wale wapuuzi
 
Huyo ndio zake toka alipokuwa waziri alikuwa na tabia ya kutoa ahadi za rushwa za wazi, wakati wa uchaguzi.
 
Simpondi ila namshauri afu nipo kwenye katiba bado maana ni haki yangu kujieleza na kuhoji.
Haki ya kujieleza na kuhoji hujaitendea haki, huenda umri wako unakuruhusu kuwaza hayo!
 
Elewa mantiki ya mtoa post, fungu la barabara ya Nyehunge limepitushwa na bunge gani, miaka mitano hujatoa ajira unakuja kuajiri kipindi hiki, hiyo ni rushwa tu.
Hata ununuzi wa ndege wapo wanadai haujawahi kufika bungeni.

Sishangai
 
Nakuuliza wewe Rais wangu Magufuli umekuwa madarakani miaka yote mitano inamaana ulikuwa huoni umuhimu wa kuvifanya hivyo vitu mpaka leo hii kipindi cha kampeni ndio utoe amri vifanyike?

Umetoa amri ya kuajiri walimu, Umetoa amri ya kujenga barabara huko kanda ya ziwa na nyingine nyingi tu sasa muda wote huo ulikuwa wapi hukufanya hivyo mpaka leo kwenye kampeni?

Kwenye suala la ajira kila mwaka bunge lilikuwa linapitisha bajeti ya ajira mpya ulikuwa hulijui hilo kweli mheshimiwa? Basi toa zile ajira zote zaidi ya elfu 46 zilizo pitishwa na bunge mwaka huu ili tuone kweli unatekeleza kweli au ndio unatuchora wapiga kura wako?

Hivi hujui na Watanzania nao wanakuchora tu kama wewe unavyo wachora hapo jukwaani kwa kuwahadaa na ajira za walimu na barabara? Watangulizi wako hayo mambo walikuwa wanayafanya kabla ya uchaguzi ndio maana watanzania waliwapa miaka 10 ya uongozi bila ubishi.

Magufuli hukupaswa leo kufanya hivi unavyo fanya leo jukwaani kwani serikali yako imekuwa ikijinasibu kila kukicha imefanya makubwa. Ni kweli mmefanya makubwa ila makubwa bila kugusa maisha ya mtu binafsi na kudili na vitu hizo ni sifa za kijinga na ndicho kinacho wakosti leo kwenye kampeni.

Leo hii mtu aliye kuwa kwa mabeberu kwa zaidi ya miaka mitatu anaonekana wa maana zaidi kwa wananchi kuliko wewe unae jiita mzalendo ambaye kwa miaka mitano yote ulikuwa humu humu ndani ukipiga kazi! Kuna tatizo sehemu.
Yeye bado ni rais na bado anapigania kazi kwa watanzania kama kipo ndani ya uwezo ni kuagiza tu .Sema na wewe akifanyiwa nini sema tu usiogope.
 
Anachokifanya yeye ni ghiriba na hadaa kwa wajinga wenzio wa Ccm. Budget circle unaanza
 
Unafiki , na uoga wake dhidi ya Kamanda na Rais mteule Tundu Lissu vinamsumbua,
Akilala akimka anawaza huyu Rais Mteule kesho atanitwanga na jiwe lipi
 
Sidhani kama kuna nchi Africa iliwahi kupata Rais wa viwango vya chini kama huyu .
 
Back
Top Bottom