Emb twende na vyote kutafuta ulinganifu.
Umesema kabla ya kuumbwa binadamu hapakuwepo na jinsia ya kike.
Twende kwenye baiolojia .
Inasemekana kiumbe binadamu ameumbwa wa mwisho. Kabla yake viumbe vyote vilikuwepo, hadi viumbe vingine viliangamia kabla ya binadamu kuumbwa, mfano dinosaurs.
Pointi hiyo ni kwamba viumbe vilikuwepo kwa jinsia mbili jike na dume, pia kifo kilikuwepo asilia kabla ya historia ya binadamu.
Hadithi za kusema binadamu aliumbwa dume peke yake,wakati teknolojia ya uzazi na vifo ilikuwepo tayari, mimi ninakuwa na wasiwasi katika kuamini muktadha mzima juu ya ukweli wa hadithi zihusuzo uumbaji wa M/Mungu zilizotungwa na binadamu kama zina chembe yoyote ya ukweli.
Umejichanganya ndugu. Mimi nimesema kabla ya kuumbwa kwa Binadamu hakukuwa na jinsia ya kike ya jamii inayojitambua kama Malaika na sio WANYAMA.
Kumbuka mada inajadili kuhusu MALAIKA.
Pia Chanzo cha habari zangu nimekitoa katika kitabu cha kale zaidi, yaani cha zamani zaidi au kitabu cha kwanza kuandikwa katika historia ya Binadamu.
Biblia takatifu ambayo ina agano la Kale na Jipya. Na sio vitabu vya hadithi kama unavyosema umevinukuu.
Biblia ni Kitabu cha Kweli na sio cha hadithi.
Ukweli na Ukale wa Biblia ndio unaofanya kuwa kitabu cha kwanza kuuzwa kwa wingi zaidi hapa duniani, kikiwa kimeandikwa katika lugha nyingi zaidi kupita vitabu vyote.
Kitabu hicho cha ukweli kinasema wazi kuwa Eva ni mwanamke wa kwanza kuumbwa, hapa hatuzungumzii wanyama.
Kabla ya ulimwengu na wanyama kuumbwa, jamii iliyokuwepo ni Malaika na Shetani. Mungu ndiye aliyekuwa muumbaji wa jamii hizo.
Hapo sasa ndipo palipokosa jinsia ya kike.
Malaika na Shetani wote ni wanaume Biblia inasema.
Ukisoma kitabu cha Mwanzo sura ya 18 utaona jinsi Mungu alivyomtokea Ibrahimu akiongozana na Malaika wawili akiwa njiani kuangalia vilio vya Sodoma na Gomola.
Wote walijitokeza katika mwonekano wa Binadamu Wanaume Watatu.
Ibrahimu akamtambua Mungu akawaandalia chakula wakala, Mungu akamwambia kuwa atamzaa Isaka.
Mwisho Ibrahimu akamwambia Mungu, Bwana ikiwa huko watapatikana watakatifu kumi je utaichoma moto Sodoma na Gomola ? Mungu akamjibu hataichoma wakipatikana watakatifu
kumi.
Labda nikuambie hivi ili uelewe.
Kabla ya ulimwengu huu tunaouona kwa macho na kuupapasa haujaumbwa, hakukuwepo jinsia ya KIKE.
Eva ni Mwanamke wa kwanza kuumbwa katika jamii inayojitambua.
Wanyama sio wanawake ni wa kike.