Simba ni mbovu na haina uwezo wa kufika robo fainal! mnaenda kupasuliwa na Wydad!Nashindwa kuelewa akili za mashabiki wa Yanga. Simba ilipodraw mechi zote mbili African football league mashabiki wa Yanga walisema Al Ahly ni mbovu, mwaka jana Simba walipotolewa na Wydad kwa aggregate kuingia nusu, walisema Wydad ya sasa ni mbovu.
Walipoona hivo wakasema Al Ahly tutampasua kwa Mkapa nje ndani, wamedraw na Al Ahly sasa wanasema Al Ahly wa moto lakini tungepangiwa kundi la Simba tungeongeza hilo group.
Wakifunga timu wanasema ipo kwenye pick wamefunga timu bora,wakifungwa wanasema pia ipo kwenye pick ya moto.
Wenzao Simba wakishinda eti wamekutana na timu dhaifu haipo kwenye ubora wake.
Mashabiki gani wa aina hii wakifungwa ooh mpira tumepiga mwingi, wameona hawatoboi kwenye kundi oooh tungekuwa kwenye kundi la Simba tungeongoza kwa point 18.
Hivi hizi ni akili kweli?
Simba kwenye hizi hatua ana uzoefu wa kucheza na mahesabu.
Simba na Yanga kila mtu kwa sasa ana probability ya kuvuka hii hatua.
Tusubiri kama nye ni bora mpige mahesabu vizuri mpite, na Simba nao wapige mahesabu halafu tuone nani ataendelea mbele.
Baada ya kupasuliwa unipe hizo hesabu zako.