Hivi Mbowe tunamlaumu kwa sababu ipi hasa?

Hivi Mbowe tunamlaumu kwa sababu ipi hasa?

Suzy Elias

JF-Expert Member
Joined
Nov 9, 2021
Posts
1,067
Reaction score
6,200
Unakuta nalalama eti Mbowe kawa kimya kisa kalambishwa asali na watawala. Unakuta namlaumu Mbowe eti ooh, katishwa kidogo tu ameufyata! Ooh, Mbowe ni TISS kuipinga serikali ni gheresha tu!

Kwangu mimi malalamiko yote hapo juu nimebaini hayana mashiko na ya kipuuzi hakika! Hivi Mbowe huyo aliyepitia magumu yote yale pamoja na kuhifadhiwa jela kwa ajili ya kuwasemea/kutusemea, ya nini tumlaumu kwa ukimya wake leo baada ya anaotutetea, kutokuwa na haja ya kutetewa?

Kwamba yeye aendelee kuumizwa kwa ajili yetu siye wajinga? Ujinga kabisa!

Mbowe kaa kimya na endelea kula raha na familia yako. Sisi ulioamua kututetea bado hatujielewi na achana na sisi, bali watawala wakikuletea asali nashauri ilambe kwa juhudi zote.
 
Hahaha..atulie ili 2025 tufanyie watu surprise. Asiwapange sana.
 
Watu wanataka wapate ukombozi kwa jasho ama damu ya mtu mwingine huku wao wakiendelea kuangalia connection, na kujadili habari za Simba na Yanga.

Kila kitu kizuri kina gharama, lazima tushirikiane ili kuipata haki nchi hii
 
Sure
 
Kesi ya UGAIDI imekuwa kitanzi kwake kukosoa mambo ya nayo endelea ya TOZO... Maana wamemshika pabaya, akikosoa kesi inafufuliwa.
 
Mbowe amepigwa "Rope A Dope".

Kachezewa kama pawn wa kumsafisha Samia ili Samia aonekane anafanya maongezi na wapinzani, wakati hakuna mabadiliko yoyote.

Kisha Mbowe hawi muwazi, anawaasa wanachama wake wawe na subira, kashindwa hata kuweka pressure mikutano ya hadhara iruhusiwe na viongozi wa CCM.
 
Watu wanataka wapate ukombozi kwa jasho ama damu ya mtu mwingine huku wao wakiendelea kuangalia connection, na kujadili habari za Simba na Yanga.

Kila kitu kizuri kina gharama, lazima tushirikiane ili kuipata haki nchi hii
Ume describe jamii ya wabongo kwa ujumla
 
Kesi ya UGAIDI imekuwa kitanzi kwake kukosoa mambo ya nayo endelea ya TOZO... Maana wamemshika pabaya, akikosoa kesi inafufuliwa.
Msikilize hapa halafu jiulize wewe umechangia nini?
 
Unakuta nalalama eti Mbowe kawa kimya kisa kalambishwa asali na watawala. Unakuta namlaumu Mbowe eti ooh, katishwa kidogo tu ameufyata! Ooh, Mbowe ni TISS kuipinga serikali ni gheresha tu...
Wanaosema Mbowe yuko kimya nimewawekea video yake post #19 wamsikilize halafu wajipime.
 
Back
Top Bottom