Mgeni wa Jiji
JF-Expert Member
- Jul 27, 2017
- 9,758
- 18,431
Wakuu mimi sina mambo mengi sana hapa najaribu kufikiria, hivi Mh. Shabiby aliwaza kweli kuwa kuna watu ambao wao wanakatwa bima moja kwa moja kwenye mishahara yao?
Hawa wataondolewaje kwenye huo mfumo aliopendekeza sababu na wao ni wamiliki wa simu watakaokatwa bima mara mbili.
Labda alimaanisha watu wakatwe ili kuchangia wengine je hii ni sahihi?, kwanini mtu alazimishwe kulipia matibabu ya mtu mwingine bila hiyari yake.
Najaribu kuwaza tu wakuu, huu mfumo sidhani kama utakuwa na tija kwa taifa, badala yake fedha tunazokusanya kama taifa.zielekezwe kwenye mambo ya msingi kitaifa na sio posho na matumizi yasiyo ya muhimu na lazima.
Kwa sekta ya utalii tu kama tukiitumia vizuri hatutakuwa na wasiwasi kwenye huduma kama afya, elimu na miundombinu. Lakini badala ya kuwaza na kutekeleza haya tunatafuta njia rahisi za ukusanyaji hela.
Haya je ununuzi wa vocha ukipungua, hizo fedha zitapatikana vipi? Je, haoni kuwa hii itapandisha gharama za vifurushi na huduma za mitandao?
Mimi ni hayo tu waungwana.