Hivi Messi ni bora kuliko Pele, Maradona, Zico, Platini?

Messi is the best footballer ktk historia ya mchezo huu wa mpira tokea uanze..!!!

They call him Magician, Messiah, the gifted, etc etc...he usually humiliates GREAT PLAYERS na kuwaaibisha kabisa...

He is very talented footballer...!!!
 
Messi is the best footballer ktk historia ya mchezo huu wa mpira tokea uanze..!!!

They call him Magician, Messiah, the gifted, etc etc...he usually humiliates GREAT PLAYERS na kuwaaibisha kabisa...

He is very talented footballer...!!!

kwa kuwa rais wangu umeongea basi mimi sina neno hapo
 
Mm binafs sijuti kutowaona pele na diego kwan huyu jamaa messi n jiniaz
 
Ni vigumu kulinganisha moja kwa moja watu waliocheza era tofauti ila kwa era yake ni bora zaidi. Kwa kuwa msemaji kawashuhudia wote na katoa mtazamo wake nadhani yupo sahihi
mkuu mm binafsi sikumuona pele platin na zico hila maradona lakini video clips zao zipo na tunaziangalia messi kweli anatisha
 
Messi is the best footballer ktk historia ya mchezo huu wa mpira tokea uanze..!!!

They call him Magician, Messiah, the gifted, etc etc...he usually humiliates GREAT PLAYERS na kuwaaibisha kabisa...

He is very talented footballer...!!!

kweli kiongozi kila aina ya jina wanampa
 
Wadau jana kwenye mechi ya fainali ya UEFA Champion nilimsikia mtangazaji wa mechi hiyo kutoka Berln kwamba amebahatika kuwaona wachezaji hao wote kwa kipindi chote lakini bado anaamini Messi ni bora zaidi.

huyo mtangazaji ni mtu mzima mwenzangu. naweza tu kusema kuwa anajua alichokuwa anakisema na alimaanisha.
 
Goli dhidi ya athletic lilikuwa balaa Baada ya messi kupokea Mpira pembeni kabisa mwa uwanja akasimama kidogo , kisha akawagalagaza jumla ya mabeki watano, ndo lilibadili kila kitu Baada ya barca Kuwa amebanwa likapelekea mechi kufunguka mwisho akabeba copa de rlay ..

Goli dhidi ya atletico Madrid la kuwazunguka mabeki na kuwapita kisha messi anapiga angle ambayo haifikiki Kwa goli keeper lilikuwa balaa na ndo limewapa ubingwa moja Kwa moja

Bayern Munich walipata dawa take mpaka dk ya 76 Kama sijakosea , pale ambapo messi alifanya vitu adimu kabisa Kwa kumpiga chenga ya mwaka boateng na kupelekea kufungua mechi barca akashinda

Return leg pale Allianz arena , messi alipikea pasi akasimama akazuga Kama haendi kokote ghafla akapiga killer pass moja matata Sana Suarez na neymar wakafanya mambo , akarudia killer pass Safari hii akapiga Kwa header jamaa wakapiga la pili mechi ikawa imeishia hapo ,

Kwa waliongalia mechi na juve mliona vision kali ya messi baaada ya kupiga pass ya juu Kwa Neymar na hapa akiwa amebadili direction ya mpira juve wakachanganyikiwa wakapigwa goli , goli la pili la barca ilikuwa nice dribble ya messi akamlamba chenga beki akaanguka akasogea Kwa kasi na kupiga shuti lililomshinda Buffon then Suarez akamalizia (hili ndo liliua kila kitu )

Penalty dhidi ya getafe mkairudie upya muone maajabu yake ( Ronaldo alijaribu kuiiga next match akakosa)

"If messi is in good mood then all oppositions tactics are irrelevant "
 
Tushukuru tu kwamba tumepata bahati ya kumshuhudia messi duniani maana hii bahat inaweza isitokee tena mpaka dunia inaisha mi shabiki wa ronaldo lkn messi ni habar nyingine kwa kwel
 
Hao wanaosema Messi mchezaji bora kuwahi kutokea watakuwa wanavuta sio bure. Mbora kwa kitu gani cha ajabu ambacho wachezaji wengine hawajakifanya? Labda kwa mchezaji mbilikimo kuwahi kutokea,hapo mm nitaunga mkono 100%
 
Jinsi ya kumzuia Messi awe nje ya uwanja tu.
Messi ni hatari hata asipogusa mpira kabla ya kukaba mpira lazima uzuie Messi asishike mpira
 
Messi huyo huyo ndie anayevunja rekodi za akina Pele na Zidane na Ronaldinho. Mpira ni zaidi ya mbwembwe uwanjani, ule mpira wa kucheza na jukwaa haupo tena siku hizi.

ndo maana nikasema ukitazama mafanikio ya haraka na ushabiki utamsifu messi anayepewa mpira na xavi ama Iniesta... kuvunja rekodi ni jambo litakalo fanywa sana kwa kizazi hiki... za messi zitavunjwa ndani ya miaka michache mno... ni mabadiliko ndani ya mpira...

kama ni mpenzi wa mpira, tazama the way hazard anavyoweza kukufanya usisimke akicheza.. wengi wanasema anaweza kuwa bora kuliko wote shida yake hataki kujivika ufalme wa kufunga magoli.... hapa ndipo kwenye tatizo.. tunauona ubora kwenye goli tu..mpira si burudani as ilivyokuwa zamani sasa hivi ni matangazo na jambo la kuleta umaarufu wa pesa na sio furaha. ndio maana messi singano analia na simba, Ronaldo anapiga mpira kwa hasira alvaro akishinda.. unaweza jiuliza kwanini Ronaldo anasusa kisa hajapewa pasi azidishe idadi ya magoli ya kupewa.? ni kwasababu akipata golden boot anapiga hela kwenye matangazo ya boxer na t-shirts za fubu(kampuni hii ipo hivi??) ...

demba ba angecheza mbele ya xavi, iniesta,beki inayoingiza mpira kama jordi na alves plus pedro na wengine katika ligi ya uhispania(rejea maneno ya mourinho juu ya ligi hizi mbili) angefunga dozen ya magoli. suarez alifunga goli ngapi katika ubora wake ndani ya liver? katika mwanzo wa kusuasua wa barca angalia katia ngapi...

kwangu ligi ya Spain ilikuwa ligi ya vitu ambavyo hauvioni premier na Bundesliga. ligi ya ujuzi wa man alone van niestroy. ligi ya ufundi wa dinho.. ligi ya Zidane.... ligi ya Ronaldo de lima...

kwenye jambo hili pengine unaweza kufananisha na mchezo wa boxing... Mayweather na manny wamefanya pambano la hela nyingi na heshima kuliko yote duniani.ndio maana Mayweather anapata jeuri yakujiona yuko sawa na Mohammed alli.. tazama ubora wa pambano fananisha na ngumi za Frazier na kina alli na mchezo wa Tyson Mike kijana... unaweza kuona nani ni nani lakini mtaani tunasema Mayweather nomaaaa... wakati kashinda kwa kuomba msaada wa kulala juu ya kamba na kukimbia kama bolt ulingoni...

messi ni bora ila atafanya kazi kunishawishi kuwa yeye ni bora kuliko okocha, kazidi utamu wa Ronaldo wawili wa brazil de lima na dinho.... kamfunika Zidane... au ye ni bora kuliko pele na maradona....
 
lumanyisa;

1. Wewe timu gani?
2. Huwa unamuangalia
3. Messi kwa mechi zipi?
Naomba unitajie mambo ambayo De Lima kafanya harafu Messi hajafanya au mchukue Zidane pia, kisha walinganishe kuanzia Assist, magoli, dribbling n.k tuone nani zaidi.
Mkuu, nimebahatika kumuona De Lima na Zidane pia ila hakuna ambae ni tishio kuliko Messi, Messi habebwi kwa promo wala matangazo yoyote yale, kama anabebwa na promo na kibiashara unazungumziaje makocha na mabebi wanaosema huyu jamaa ni hatari!?
Huyo Iniesta na Xavi hawamfikii hata Messi kwa Assist.
4. Ni wewe ndo unamfabanisha Messi na De Lima kwa kumuweka Level moja nae ila magwiji wa soka hawajawahi hata kufikiria kwamba De Lima amecheza au kufikia kiwango cha Messi.
 
Last edited by a moderator:
"If messi is in good mood then all oppositions tactics are irrelevant "
AKON hapo umeua sana aisee......eti mi namuona wa kawaida tu
 
Ni kipi De Lima kafanya ambacho Messi hakiwezi!?

unataka matukio? hakuna njia nyingine ikiwa ni matukio angalia Ronaldo wa Barca kisha.. wa inter kisha Madrid... tazama uwezo binafsi wa phenomena.

kucheza mpira hata mchangani watu wanacheza ukisema kipi Ronaldo kafanya messi kashindwa huku ukiwa na moyo wa kuwa yeye ni mchezaji na Ronaldo ni mchezaji bila kuwaangalia wote wawili utakuja na jibu rahisi.

ila labda nikuulize uzuri mpira kwako unaupima kwa lipi?
 
Yawezekana kabisa messi si wa kawaida!na maradona na pele hawajawahi kusemwa kama ni wachezaji wa sayari nyingine,,,messi anasemwa hivyo!!bbc kwa sasa wanamwita Magician Messi
 
Messi!?.. Kujitafutia dhambi tu huko... Kiumbe wa ajabu huyu..
 

wabongo bana yani umeulizwa swali baada ya kujibu nawe unauliza swali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…