A
Anonymous
Guest
Wananchi tunahitaji ufafanuzi kuhusu nguvu na utendaji wa Mgambo wa Jiji, hususan katika eneo la Kariakoo, wakidai kuwa kumekuwa na ukamataji wa mali za wananchi unaosababisha kero kubwa.
Baadhi ya waendesha pikipiki wanakamatwa bila kupewa nafasi ya kujieleza au kusikilizwa, huku pikipiki zikichukuliwa hata katika mazingira ambayo tunaona hayana makosa ya msingi.
Aidha, wafanyabiashara ndogondogo (machinga) nao wanakamatwa mara kwa mara wao na bidhaa zao, ukienda katika baadhi ya ofisi za Jiji eneo la Kamata utakuta vyumba vimejaa bidhaa zilizokamatwa, huku maeneo kama Anatogo kukiwa na pikipiki na bajaji nyingi zilizokamatwa.
Hali hiyo imekuwa ikiwasababishia hasara na maumivu makubwa kiuchumi, tunahoji iwapo maelekezo ya viongozi wakuu wa Serikali kuhusu kutokamata au kuchukua mali za wananchi bila kufuata utaratibu hayawahusu watendaji wa Kariakoo? Kama alivyoelekeza Waziri Mkuu hivi karibuni!
Pia soma ~ Halmashauri ya Jiji Dar: Hatukamati Wanaoshusha au kupakia abiria bali wanaoegesha kabisa
Mamlaka husika zifuatilie suala hili na kuhakikisha ukamataji wowote unafanyika kwa kuzingatia sheria, haki na taratibu zilizowekwa.