Hivi Michael Jackson alikuja Tanzania na kugoma kushuka uwanja wa ndege na kusalimiana na Mzee Mwinyi kisa Tanzania hewa yake ni chafu?

Huwa nikiangalia MJ alivyotumia talanta yake kuusaidia ulimwengu huu na kufikisha jumbe na prophecies lkn watu wanavyokuja kumchafua ndipo nakumbuka duniani hapa jipiganie ww tu na labda circle yako.

Ngoma kama Earth song, ile ni prophecy, we're the world, heal the world, hamna msanii dunia hii aliofanya hayo. Lkn leo hii MJ anaonekana kama alichukia weusi na masikini wakati alikua ni mtu mwenye upendo sana kwa wasio jiweza
 
Hamna lolote. Hizo ni story za vijiwe vya kahawa. Michael Jackson ana mtindo wa kuvaa barakoa tokea huko US.

Sehemu nyingi anapokwenda huwa anafunika uso wake na barakoa sasa waswahili wakaona kuwa hiyo ni ishara ya kuzuia harufu mbaya wakatunga uongo wao.

Michael Jackson hana hizo dharau za kwenda sehemu na kuwaponda wenyeji wakati amekwenda kujichanganya na watu vijijini huko.

Hizo ni story za uvumi na si kweli.
 
Kama uliisikiliza vzuri Earth Song alikua anamlaum Mungu.
 
Kilichoripotiwa na vyombo vya hbari wakati huo ndo hicho.
 
Kwani alikuja Tanzania kuongea na Mwinyi, yule ni mwanamziki alialikwa kuja kuimba, kuna picha yoyote anaimba ? Yule mbana pua alikatisha ziara
 
Hata mm hiyo story niliisikia, na ndo nilielewa hivyo hadi leo kabla sijaiona hii picha.
 
Vijana wa siku hizi wanapenda sana kueneza taarifa za uwongo bila hata kuzichambua kwanza kabla ya kuzieneza; Huyu alieanzisha thread hii tayari naye anachangia kusambaza taarifa za uwongo. Kama MJ hakushuka kwenye ndege hiyo picha aliyopiga na Mwinyi walikuwa wapi.

MJ alikuwa na tabia ya kuweka face mask (bala ya korona) kuzuia hewa ya vumbi hata aakiwa Marekani. ALipokuja Tanzania alikuwa na face mask hiyo, ambayo alikuwa akiivua anapokutana na viongozi wa serikali kama anavyookena kwenye picha hiyo na pia alipopokelewa na Hassan Diria aliyekuwa Waziri wa Mambo ya nje wakati huo

 
alibana pua kwa sababu msimu anakuja ulikua msimu wa joto kali. na kipindi cha joto kali hewa huwa ni thick. hiyo ilikua ndio sababu ya yeye kupata shida ya kuvuta hewa ikaonekana akishika pua yake na athari zaidi ni pua yake vile ilikua imefanyiwa surgery.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…