Mimi sio mtaalamu wa magar na pia ikumbukwe tu kuwa hapa fb ni. Kisima cha elimu.
Huwa ninashangaa sana mtu yoyote akiwa mjuvi wa mambo au anaelezea kitu fulani then akashindwa kutoa suluhisho ili kumalizia kazi yake nzuri ya kutoa elimu.
Nimefurahi kupata elimu hii ya magari, na pia hasa hasa kuhusu engine kuchoka na vitu muhimu ni engine na oil seal.
Nina swali, iwapo mtu kanunua gari na akafanya moja ya mambo yafuatayo :-
1: akanunua engine mpya japokuwa tunasema ni used from Japan na akaweka hasa hasa kwa magari madogo, je. Life span yake itaongezeka?
2: iwapo atanunua original engine seal, je life span ya gari itaongezeka?
3: vipo vitu vingine mtu akiamua kwenda mbali kutaka kuongeza life span ya gar mfano kununua half engine hasa hasa sehemu ya gearbox, kufanya matengenezo kama ya miguu kuanzia bearings, hub,, then kusafisha rejeta, engine oil mpya original, kuweka maji yake original, kusafisha air cleaner na mengineyo madogo madogo, je haiwez kuifanya gari kuwa katika kiwango cha sawa na mpya au kuwa katika Hali nzuri na kuiongezea life span yake?
Nb. Hapa namzungumzia magari madogo kama vitz, starlet, ist, vyenye engine isiyozidi cc 1490 na spear zake zipo kwa wingi na pia gharama zake ni affordable.