Hivi mishahara kwenye NGO za kimataifa huwa ni kiasi gani?

Hivi mishahara kwenye NGO za kimataifa huwa ni kiasi gani?

Mfano NGO kama DANIDA, SIDA na nyingine za aina hiyo huwa wanalipa mishahara kiasi gani kwa nafasi let's say kama ya Finance officer?
Mshahara unakua bargainable kutokana na qualifications, experience pamoja na skills.

Mtu mwenye working experience ya 5yrs atalipwa tofauti na mtu mwenye experience ya 10+ yrs.
 
Hyo ni serikali sio private
hiyo ni just a code ila inatumika katika kuchanganua mishahara yaya watumishi wa serikali wanaofanya kazi wizarani, ofisi za mikoa na halmashauri isipokuwa walimu na afya.
Kuna taasisi kibao za serikalI zina code tofautitofauti zinazochanganua viwango vya mishahara ya taasisi zao.
Hiyo sio SI unit kwamba lazima ifanane kila taasisi
 
Duh.kwani wao hawatumii scales za TGS?
hiyo ni just a code ila inatumika katika kuchanganua mishahara yaya watumishi wa serikali wanaofanya kazi wizarani, ofisi za mikoa na halmashauri isipokuwa walimu na afya.
Kuna taasisi kibao za serikalI zina code tofautitofauti zinazochanganua viwango vya mishahara ya taasisi zao.
Wao nao watakuwa na code zao
 
Ni mikubwa lakini ndo hivyo unataumika mbwa yaani wanakukamua hasa kama ganda la muwa. Ni za mkataba bidii yako ndio mkataba wako. Hazina rushwa kupata bali kichwa chako, wanaangalia zaidi brain kuliko vyeti, cv yako mtaji wako, hazina urefu wa kamba, safari sana, nyumba, usafiri, bima, nk
 
Ingia page ya UN hata nyingi international firm Wana rate za mishahara yao ukiingia kwenye website zao
 
Ni mikubwa lakini ndo hivyo unataumika mbwa yaani wanakukamua hasa kama ganda la muwa. Ni za mkataba bidii yako ndio mkataba wako. Hazina rushwa kupata bali kichwa chako, wanaangalia zaidi brain kuliko vyeti, cv yako mtaji wako, hazina urefu wa kamba, safari sana, nyumba, usafiri, bima, nk
ungejua, wala hawatumiki unavyofikiria na wala hakuna kazi za pressure kinachomatter ni pprofessionalism na nidhamu ya hali ya juu manake huko ni kujisimamia mwenyewe tu kazi unaletewa kwenye email ni wewe kujisimamia usivuke deadline
Mazingirza mazuri ya kazi kuanzia ofisi hadi vitendea kazi,muda mfupi wa kazi mashirika mengi unakuta kazini ni kuanzia saa 3 hadi 10 tofauti na hapo labda kuwe na kazi maalumu, unapewa gari la ofisi unajiendesha mwenyewe ,unaweza ukafukafanya kazi toka home, mwanamama akijifungua likizo ya uzazi miezi 4 ,mishahara 13 kwa mwaka , unasomeshewa watoto.
Mishahara ni mikubwa kwa sababu ya mishahara inayolipwa kwao ni mikubwa huku napo hawataki kuwa chini sana
 
Mfano ipo migodi unakula pesa nzuri plus mda wa kutosha kupumzika.
Mnapiga Kazi fully kambini wiki 6 then unaenda kupumzika wiki tatu, waliokuwa mapumzikoni wanarudi kazini nyie mnaenda off wiki 3 kurefresh.
 
Ni mikubwa lakini ndo hivyo unataumika mbwa yaani wanakukamua hasa kama ganda la muwa. Ni za mkataba bidii yako ndio mkataba wako. Hazina rushwa kupata bali kichwa chako, wanaangalia zaidi brain kuliko vyeti, cv yako mtaji wako, hazina urefu wa kamba, safari sana, nyumba, usafiri, bima, nk
Nimemaliza interview muda mfupi uliopita,jamaa wako Well organised.ila tu interview zao ni ndefu,tumetumia almost lisaa lizima.
 
Back
Top Bottom