Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ile ni mito au mifereji ya maji taka!!?Wakuu hivi mito kam Msimbazi, Mzinga nk, ina samaki? Imewahi kuwa na samaki? Ningependa tu kujua.
Nenda Mbagala Mzinga, ukauziwe kambare fresh!Wakuu hivi mito kam Msimbazi, Mzinga nk, ina samaki? Imewahi kuwa na samaki? Ningependa tu kujua.
i second thisSamaki wapo ila wa kiduwanzi tu.niliwao ona jamaa anavua kambale pale mto msimbazi.
Pia baadhi ya mifereji kama ya mikocheni na msasani ina kambale sana especially misimu ya mvua
Sent from my CPH1803 using JamiiForums mobile app
Ina MATOMBOLILOWakuu hivi mito kam Msimbazi, Mzinga nk, ina samaki? Imewahi kuwa na samaki? Ningependa tu kujua.
Zipo ndogo ndogo kiasi ila kambale ndio nimeona wengi sanaWakuu hivi mito kam Msimbazi, Mzinga nk, ina samaki? Imewahi kuwa na samaki? Ningependa tu kujua.
Miaka ya nyuma ule mto ulikuwa na samaki, kambale na perege na watu walikuwa wanavua kwa kitoweo lakin baada ya watu kuvamia ule mto kwa kuanza kujenga makazi pembezoni mwa mto na kutiririsha maji machafu ya vyooni mbaya zaidi kuna kiwanda cha nguo kinaitwa NIDA kama sijakosea kipo Tabata nacho kikaanza kutiririsha maji machafu ya kiwandani during those days nilikuwa nasoma primary na njia yngu kubwa kwenda/kurudi shule ilikuwa pale darajani nilishuhudia vijana wengi wa maeneo yale wakiopo hao samaki waliokuwa wanakufa kwa sumu ya maji ya kiwandan since then nadhan samaki ndio waliishia pale mpaka namaliza std 7 nikiwa napita pale nikawa nashuhudia mabadiliko ya rangi ya maji tu mara blue, red, black and etc. Sijui NEMC walikuwa wapi wakati ule na mpaka sasa sijui wapo wapi😣😣,!!! Lile bonde kabla halijaathiriwa na uchafuzi wa mazingira nakumbuka walikuwa wanalima sana mpunga na mchichaKwa jinsi ilivyo michafu hata Samaki wenyewe wameghairi kuishi humo.
Ule Mto pale Kigogo mwisho ukipita SAA 9:30 unakuta maji mekundu, SAA 11:00 maji ya Buluu, SAA 13:32 maji meusi, SAA 15:02 maji mekundu, SAA 16:13 maji ya Njano.
Sasa hapo Samaki gani mjinga atakubali kuishi kwenye maji yanabadilika badilika kama Kinyonga?