Mbunge wangu yupo huko yapata miaka minne nilimwona mara ya mwisho Kijijini akiwa kwenye kampeni akijinadi na kutaka Kura yangu!
Amepata Uongozi sasa na Familia kaihamishia huko mjini!
Ile nyumba yake aliyokuwa anaijenga kijijinihaitaki tena anasema amepata kiwanja (Open Space) Pale Masaki hivyo atasimamisha mjengo huko!
Watoto wake tuliokuwa tunasoma nao pale Shule ya msingi Mchungwani wamehamishiwa International school kule kenya!!
Anasema hatarudi mjini na sasa kwani yupo busy na Viongozi wenzie kuangalia namna ya kujenga flying Over hapo Mjini Dsm!!! Bora Nije nikae huko alipo mbunge wangu aliyepata madaraka baada ya kura yangu kumchagua!...... NISIJE MJINI WAKATI KIONGOZI WANGU YUPO HUKO MWAKA WA 4 SASA? HAINIINGII AKILINI NAKUJA HUKO HUKO MJINI!!!