Kama wewe ni mwenzangu na Mimi tunaopambana anagalao tufike sehemu nzuri, kuna ile unawatazama waliofanikiwa na mbilinge zao za maisha unaishia kusema hakika utajiri ni Ngumu.
Just see few Case studies
- Mtu ana mabasi 7 isitoshe amechukua mkopo mrefu benki, marejesho kila mwezi bahati mbaya basi tatu zinakula mbanga bila kutarajia. Lakini cha ajabu unamkuta tajiri ana kula maisha party after party hawazi.
- Kuna wale matajiri waliofilisiwa kipindi cha JPM kwa makosa ya uhujumu uchumi. Mali zao nyingi zilitaifishwa but tuna kutana nao as if nothing happened 😁😁 na wanapambana kama hamna kilichotokea.
Kuna wenzangu na Mimi unapambana unapata hela kiasi flani unaanzisha mradi wako bahati mbaya ukifeli na wewe umefeli na inakuwa ni simulizi ya Karne kwa kila mtu 😁😁😁
Hakika nihitimishe kwa kusema maisha ni fumbo gumu sana ndugu zangu.