Hivi Mkurugenzi mmoja wa halmashauri kukaa kituo kimoja kwa zaidi ya miaka 3 hakuwezi kuwa sababu ya kutengeneza ufisadi?

Huwezi kurekebisha kila kitu Wacha wazipige
 
Hata siko serikalini mkuu,
Ila harakat zangu nafanya kazi sn na watu wa serikalini, hasa hao wakurugenzi.

Hebu acheni chuki za kijinga,number hazidanganyi,jamaa mchapakazi sana[emoji4]
Ndo maana unamtetea jamaa wako huyooo, ukute ana sifa mbaya wee unampamba tyuuh, binamu acha hizo bhana
 
Unajua ni magari mangapi yapo juu ya mawe na madereva baadhi wamekaa tu bila ya majukumu kwa zaidi ya miaka 2!?.Unajua kuwa kuna magari yapo gereji mwaka 4 sasa na baadhi yalilipiwa pesa lakini hazikufika!?.
Huyo mtu wako anajificha katika hayo unayo sema,lakini ndani ya ofisi kuna ufisadi mkubwa kupitia hao maafsa aliowatengene,na nikawaida kuwa mstari wa mbele kumtetea kama ufanyavyo.
Serikali ina ajiri mtumishi ili akafanye kazi kwa mujbu wa kanuni na sheria za kazi na ndipo alipwe mshahara.Sasa wewe unaona ni sahihi mtumishi kuondolewa katika nafasi yake na akabaki kusaini tu kitabu cha maudhurio asubuhi na mchana kisha anakaa tu bila ya kazi na huku anaendelea kulipwa mshahara?.
 
Hahahaaa!Tupa jiwe giza ukisikia yalaa!Jua tayari.Bila shaka wewe ni sehemu ya mwanamtandao wake,umizeni tu watumishi wengine kwa hongo mnazopewa ili kupitisha dili zenu.Ila hipo siku mtakuja hungama.
Pole Sana mkuu

Ebu acha chuki zako tujenge taifa letu

Una tuhuma dhidi yake weka ushahidi mezani, Sio kuzusha Maneno ya uongo kumchafua bure jamaa.

Ushahidi wangu nmeshakupa tayar
-fuatilia makusanyo mapato ya ndani ya mkoa,halmashaur Yake iko namba ngap.

Kashusha ushuru na tozo kandamizi ili Watu walipe waache magendo,sahv Unalipa ushuru wako Safi na hatukimbizani Tena na polisi Kama zamani.

-fuatilia matokeo ya kielimu kuanzia STD 4,7 Hadi form 4,halmashaur Yake iko namba ngapi kitaifa.
Walimu walevi,watoro na wazembe anawanyoosha kweli kweli.

Mwaka Juzi naskia Kuna mtendaji kalewa kilabuni kaibiwa ushuru na mashine ya risiti,mkurugenz kamfuma kamlamba sticky Kama mwanafunzi[emoji1787]

-Fuatilia response ya wakulima na wafanyabiashra waliowekeza kwny halmashaur Yake Ni Kias gani anakubalika.

Halmashaur Yake ukiwa mwekezaji na mdau wa maendeleo unanyenyekewa mno.

WATUMISHI WAZEMBE NA WAPIGA DILI MNATESEKA SANA AISEE[emoji4]
 
Hata siko serikalini mkuu,
Ila harakat zangu nafanya kazi sn na watu wa serikalini, hasa hao wakurugenzi.

Hebu acheni chuki za kijinga,number hazidanganyi,jamaa mchapakazi sana[emoji4]
Mkuu!Gari inaweza kuendelea kukaa gereji mwaka mzima ili hali pesa ya matengenezo ilitolewa kesh?.T.O na madereva wake wa wili wote wamekalishwa benchi kwa zaidi ya miaka 2 sasa na huku wakilipwa mishahara,kwako wewe hii hipo sawa?.
 
Ndo maana unamtetea jamaa wako huyooo, ukute ana sifa mbaya wee unampamba tyuuh, binamu acha hizo bhana
Binamu,
Kwny harakati zangu Nmefanya kazi na wakurugenzi wengi sn Hapa nchini.

Hasa kwny biashara za mazao,
Changamoto kubwa Ni watumish wa chini kua POA POA na mkurugenz, urasimu kila Kona.

Unanyanyasika Sana maana huna pa kusemea,wote mkurugenz,watumish Ni usumbufu,urasimu na rushwa Kwenda mbele.

Sasa halmashari ya jamaa,Yuko very strict na hataki konakona na urasimu kwa wadau wake wa maendeleo.

Ndo maana hata akiwa na Jambo lake,
Response ya wafanyabiashara,wakulima na wadau wa maendeleo iko chap Sana[emoji4]
 
Mkuu!Gari inaweza kuendelea kukaa gereji mwaka mzima ili hali pesa ya matengenezo ilitolewa kesh?.T.O na madereva wake wa wili wote wamekalishwa benchi kwa zaidi ya miaka 2 sasa na huku wakilipwa mishahara,kwako wewe hii hipo sawa?.
Hayo Mambo yenu ya ndani wafanyakazi wake ata siyajui,nadhan mna vikao vya ndani, mkae myaongee myamalize.

Jamaa mbona msikivu sn, japo ubabe Kias flan anao, pale akitaka kuforce jambo lake lipite.

Binafs nmeongelea kwa general view, Kwa niliyoyasikia na kwa jinsi nilivofanya nae kazi na navomjua.

Ila takwimu za performance yake kiujumla hazidanganyi,ndo maana kaaminiwa kukaa pale MDA mrefu hivo
 
Mkuu!Gari inaweza kuendelea kukaa gereji mwaka mzima ili hali pesa ya matengenezo ilitolewa kesh?.T.O na madereva wake wa wili wote wamekalishwa benchi kwa zaidi ya miaka 2 sasa na huku wakilipwa mishahara,kwako wewe hii hipo sawa?.
Ila si mnalipwa lakni nikafikiri mnakaa benchi na hamlipwi daah πŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒ


Labda na yeye kasomea hayo mambo anawapunguzia majukumu,

Ishini na Mkurugenzi wenu vizuri ndio boss wenu
 
Hawa wanawivu tu, huyo T.O ajue kua mkurugenzi ndio boss wake akisema a na yeye aitikie a ukienda beyond hapo anaishia kujuta kama hivi

Aishi na mkurugenzi kwa akili ata enjoyπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚


Tatizo ujuaji mwingi ndo unaponza
 
Kwako wewe ni sawa dereva muajiriwa hanyimwe gari ila ndugu yake asiye muajiri na wala hana mkataba apewe gari?.
 
Ungeenda kuweka kwenye post ingekuwa jambo jema coz sio kila mtu atapitia COMMENTS zote kutafutiza kama kuna mtu kataja. Mtoa POST angeweka kwenye UZI wake
Tatizo Mtoa mada kaileta kimajungu zaidi,

Ile kutupa jiwe gizani, mtandao Kama jf hayo Mambo yashapitwa na Wakati, alipaswa aweke wazi ili asaidiwe tatizo lake.

Kumbe tatizo lake Ni Madreva waliosimamishwa kazi kwa uchakavu wa magari uko gereji[emoji4]
 
Huyu atakuwa T.O bILA CHAKA
 
Hawa wanawivu tu, huyo T.O ajue kua mkurugenzi ndio boss wake akisema a na yeye aitikie a ukienda beyond hapo anaishia kujuta kama hivi

Aishi na mkurugenzi kwa akili ata enjoy[emoji23][emoji23][emoji23]


Tatizo ujuaji mwingi ndo unaponza
Kabisa,
mtoa mada tatizo lake nadhan liko hapo

akae vzur na boss wake wayamalize

Hapo huenda Ni kutunishiana misuli,

Transport officer anasema
"utanifanya Nini boss,ushahidi hamna?"

Boss anasema,
"Hutaki kufuata maelekezo yangu,kazi sikufukuzi, wilaya sikuhamishi, utakaa benchi usome magazeti asbh Hadi jioni,uishi kwa mshahara tu mwezi Hadi mwezi"

Ujue nnavowajua Madreva wa serikali
Ni wazee wa maadili ya vifusi,michanga,posho za safari,n.k.

Gari ikikaa MDA mref sn gereji na hujazoea maisha hayo ya kutegemea mshahara tu, month to month ni hatar sana

Njaa inauma balaa,
Hata pesa ya bia au kuhonga upati[emoji1]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…