Hivi Mkurugenzi mmoja wa halmashauri kukaa kituo kimoja kwa zaidi ya miaka 3 hakuwezi kuwa sababu ya kutengeneza ufisadi?

Unabishana lete ushahidi mezani,nami ntaweka wa kwangu mezani, kwa hoja zangu zote nilizoorodheaha hapo. twende kwa numbers mkuu [emoji4]
Weka huo ushahidi wa wakulima kupewa pembejeo na hapo halmashauri.Kilichofanyika katika msimu wa kilimo ni kule kujiandikisha kwa ajili ya mbolea ya ruzuku kama ulivyokuwa mpango wa serikali kwa nchi nzima.
Kitu kingine ilikuwa ni kutoa sumu ya kuua wadudu wahsribifu wa mazao ikiwemo panya,na sumu ililetwa na wahisani na iligawiwa karibu halmashauri zote za mkoa wa Morogoro.

Haya hicho kilochotolewa na halmashauri kama halmashauri ni kipi?.Kiweke hapa.
 
Unabishana lete ushahidi mezani,nami ntaweka wa kwangu mezani, kwa hoja zangu zote nilizoorodheaha hapo. twende kwa numbers mkuu [emoji4]
Kwa kupitia T.O wa mchongo,pesa kuanzia za matengenezo ya gari,mafuta,vipuri n.k zinapigwa na magari ni mabovu siku zote.Utaratibu wa kisheria wa ukaguzi wa magonjwa ya gari na matengenezo haufuatwi tena na gari zinatengenezwa mitaani kwa gharama ndogo huku zimetolewa pesa nyingi.

Acha kukwepa kusudio la uzi.
 

Mkuu, mara zote kitanda usichokilalia daima huwezi kujua kunguni wake.
Watumishi wa mahala husika ndo wanaomjua vizuri mkuu wao. Wewe na Boss wao kuna mambo yanayowakutanisha, maslahi ya Serikali na maslahi binafsi.

Mkurugenzi yupo kuhakikisha miradi ya maendeleo ndani ya Halmashauri yake inafanikiwa kupitia aidha mapato ya ndani ama Serikali kuu. Hicho ndicho kipimo cha ufaulu wake, sasa unategemea azinguane na wawekezaji na wadau wake wanao mletea mapato kwa ajili ya maendeleo? Atapimwa kwa kitu gani?

Mtoa mada anaweza kuwa sahihi ama asiwe sahihi, ingawa mara nyingi maslahi hufifisha kanuni na taratibu za jambo husika, na hiki ndicho chanzo cha kutokuelewana baina ya bwana mkubwa na watu wake wanaosimamia kanuni na sheria pasipo kupindisha. Substitution inaweza kufanyika ili uchezwe mdundo sawa, ngoma iflow pasipo vikwazo.
 
Mh:Rais na mama wa taifa,
Asante sana na pongezi sana kwa mabadiliko haya ya wakurugenzi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…