Hivi mnafanyaje kuishi na mtu anayenuna?

Achaneni nae,. Sio tu kununa Sometimes inatokeaga tu mtu hujiskii kuzungumza zungumza na watu
Miezi miwili anajisikia, mwezi wa tatu hajisikii!
Huu ni utetezi au umeshindwa kuchambua mantiki ya mleta mada?
 
Hiyo tabia huwa inaambukiza,muhimu ni kuwa positive wakati wote,usikubali uhuzunike kwa sababu yake,magonjwa ya kitabia nayo ni mengi sana na hayazungumziwi.
Kwel mkuu kwani naona hata sisi tumeanza kuingia kwenye huo mtego wa kumnyamazia bila kumsemesha kitu ambacho bunafsi kinatuuma sana
 
Mwanaume kununa maana yake wewe ni dhaifu.

Unaogopa makabiliano(confrontation)

Kama anaogopa kukabiliana na nyie, kabilianeni naye, muulizeni shida nini

Mwanaume kununa maana yake wewe ni dhaifu.

Unaogopa makabiliano(confrontation)

Kama anaogopa kukabiliana na nyie, kabilianeni naye, muulizeni shida nini
Tumejaribu kumuuliza amesema hakuna tatizo. Ila mkuu ulivyosema kuogopa makabiliano nahisi labda jamaa anahiyo tabia pia. Mnaweza kuwa mnajadili jambo katika Hali ya kawaida,yeye akichangia mkaja kumrekebisha kwa Nia ya kuweka usahihi kwenye hoja yake anaanza kubadilika na kukaa kimya hadi mmalize mada. Sasa kwa kuwa hatujui chanzo Cha mnuno wake tunajikuta tunapapasa hata sababu za hovyo kama hizo.
 
Atakuwa anewasikia wakati mnamsengenya! Wanaume kama mabinti, mnakaa kusengenyana?
Japo hilo halijawahi kutokea ila hata lingekuwepo dawa ilikuwa kufunguka kuwa jamaa zangu nimewasikia mnanisema moja mbili,sijapeda. Kununa ni suluhisho kivipi?
 
Hii nayo ni hoja ya Msingi ambayo kwenye kutafuta sababu inabidi tuiongeze na kuitafakari
Amegundua kuwa "nyie sio type yake" ndio maana anajitenga nanyi. Hapo mwanzoni mlikuwa bado hamjajuana vema, ila sasa mmejuana na kila mmoja achukue 50 zake..
 
Angekuwa mwanamke tungesema ishi nae kwa akili,kwa kuwa mwanaume akipita kulia ww kushoto mpotezee
 
Kwa mujibu wa maelezo huyo itakuwa ana matatizo matatu.

1. Upwiru
2. Upwiru
3. Upwiru
 
Mpelekeni haraka kwa Mwamposa akaombewe. Ni pepo tu hilo ndilo linalo msumbua.
 
Ameachwa na mmoja wenu
 
Mmletee ufala halafu awachekee tu.

Muombeni msamaha mlipomkosea maisha yaendelee, maana inavyoonekana ni mtu wa muhimu kwenye hiyo kazi yenu ndiyo maana mnaumia na kununa kwake
 
Mmletee ufala halafu awachekee tu.

Muombeni msamaha mlipomkosea maisha yaendelee, maana inavyoonekana ni mtu wa muhimu kwenye hiyo kazi yenu ndiyo maana mnaumia na kununa kwake
Maana ya timu nikwamba kila mmoja ana umuhimu wake ili kufikia malengo yakazi,hivyo hakuna mwenye umuhimu kuliko mwingine. Tufanye labda tumemletea ufala kama unavyohisi, dawa nikununa au alitakiwa aseme kilichomkwaza watu wayamalize kiume?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…