Wakuu salaam kwenu. Imebidi niombe maoni yenu kwani Kuna tabia za ajabu ambazo kuishi nazo yataka moyo.
Tumepiga kambi kwa kazi Fulani ya miezi sita Mimi na jamaa zangu watano,hivyo tupo jumla watu sita, wote wanaume.
Tunaishi maisha ya furaha kama marafiki au niseme ndugu kwani hakuna mwenye tatizo na mwenzake. Wiki mbili zilizopita mwenzetu mmoja kaanza Kununa haongei na wenzake kama zamani.
Salamu ni mpaka umuanze ndo atakujibu Kisha anaendelea na mambo yake.Hii Hali imetusumbua sana kwani hatukuzoea kumwona akiwa hivyo.
Tumejaribu kumuuliza nini shida anadai yupo sawa na majibu yake ni yamkato kuonyesha anahasira Fulani. Hii kazi imebakisha miezi mitatu lakini furaha iliyokuwepo mwanzo imetoweka kwani hatujui mwenzetu nini kimemkuta.
Mnaishije na watu wa aina hii na ukizingatia ni mwanaume baba mwenye familia yake kabisa?