Hivi mnawezaje kuangalia mechi bila sauti?

Hivi mnawezaje kuangalia mechi bila sauti?

SAYVILLE

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2010
Posts
7,895
Reaction score
12,975
Kuna wakati huwa najaribu kwenda chimbo tofauti, ukiacha na zile zenye hadhi ya vibanda umiza ili kucheki mechi, moja ya jambo lililonishinda ni kuangalia mpira bila sauti ya mtangazaji na mashabiki wa uwanjani.

Mfano kuna chimbo moja nilitokea kulielewa ila kilichofanya niache kwenda eti wanaweka sauti ya mechi kipindi kimoja tu. Kipindi cha pili wanamute sauti ya mechi wanaweka muziki eti ili wale wateja wao ambao hawajaja kuangalia mpira nao waridhike. Kuna siku nikaona huu us*g sasa, half time nikarudi zangu kumalizia game nyumbani. Nadhani ile ilikuwa mara ya mwisho kwenda pale.

Kuna chimbo lingine, nilikuwa nakwenda wakati fulani. Siku moja Simba na Yanga zote zikawa zinacheza. Screen moja ikawa mechi ya Simba nyingine ya Yanga. Nadhani ilikuwa ile ya Power Dynamos na El Mereikh. Pamoja na kwamba vibe lilikuwa la kutosha siku ile ila kitendo cha kuswitch sauti kwa kuweka sauti ya mechi moja kwa kipindi kimoja kilinikata stimu kabisa siku ile.

Kuna chimbo lingine la kishua, hao wana mascreen kama yote ila kwa kuwa wanaonyesha mechi nyingi kwa wakati mmoja, wao wanaona hata wakiweka sauti za waimbaji wa karaoke waka mute sauti za mechi zote kwao ndiyo suluhisho la tatizo hili.
 
Kuna sports Cafe na pub, pub ni sehemu ya kupombeka na vibe la muziki, hizo kuonesha mechi NI bonus tu.

Yani mtu aache kuwafurahisha wateja wake wa kila siku Kwa ajili ya mtu anayekuja kuangalia Mpira tu halafu ananunuwa soda moja au maji dakika 90.

Hii mipira muwe mnaenda kwenye Mabanda umiza pub ni sehemu ya shangwe siyo kuleteana stress za Mpira.
 
Back
Top Bottom