Hivi Mo Dewji akipokea laki moja kimakosa hawezi kukimbia kwa wakala kuitoa?

Hivi Mo Dewji akipokea laki moja kimakosa hawezi kukimbia kwa wakala kuitoa?

MSAGA SUMU

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2015
Posts
6,661
Reaction score
21,656
Tuseme bilionea yupo asubuhi ofisini anaendelea na majukumu Mara ghafla inaingia laki moja kwenye simu kimakosa, je hapa bilionea hawezi kuacha shughuli zake na kuchukua lifti kwenda kwa wakala kuwahi kuitoa?

Hapa tunaongelea bilionea anayewalipa wafanyakazi wake wa viwandani chini ya laki 2 kwa mwezi.
Hawezi kuchukua hii na ikamsaidia kidogo kwenye mambo yake?
 
Tuseme bilionea yupo asubuhi ofisini anaendelea na majukumu Mara ghafla inaingia laki moja kwenye simu kimakosa,je hapa bilionea hawezi kuacha shughuli zake na kuchukua lifti kwenda kwa wakala kuwahi kuitoa?
Hapa tunaongelea bilionea anayewalipa wafanyakazi wake wa viwandani chini ya laki 2 kwa mwezi.
Hawezi kuchukua hii na ikamsaidia kidogo kwenye mambo yake?
ukimbie kwanini ? uvunjike miguu au ugongwe na baiskeli bure tu kwaajili ya laki moja ambayo hujaitolea jasho? hapana usifanye hivyo, wala MoD hawezi fanya hivyo coz hujui alokosea kanuia nini na hilo jasho lake lililokosea njia.
 
Kuna watu tu sio waungwana,hyo n tabia tu hata hvyo kutumia visivyo halali n kujitaftia matatizo tu
 
Unaongelea mtu mwingine badala ya kujiwazia wewe?
Mnaolalamika kulipwa laki mbili na MO kwani mmelazimishwa kufanya kazi kwake?

Ukiona pesa ndogo acha kafanye kazi kwingineko.
 
Hela zake zenyewe zinaingiaga tu so inawezekana akajua ni ya biashara hana muda wa kusoma hata ni shingapi insignia yeye ni kucheki balance tu na tena ana wahasibu special kwa kazi hio
 
Mo Dewji ni taasisi hata mawasiliano yake yapo kwa mfumo wa taasisi.. Kuna namba ukituma hela haiendi kamwe.
 
Tuseme bilionea yupo asubuhi ofisini anaendelea na majukumu Mara ghafla inaingia laki moja kwenye simu kimakosa,je hapa bilionea hawezi kuacha shughuli zake na kuchukua lifti kwenda kwa wakala kuwahi kuitoa?
Hapa tunaongelea bilionea anayewalipa wafanyakazi wake wa viwandani chini ya laki 2 kwa mwezi.
Hawezi kuchukua hii na ikamsaidia kidogo kwenye mambo yake?
Kwenye mambo ya kijinga na mawazo ya njaanjaa ndiyo Mo unamtolea mfano?
 
Ubahili ni sehemu moja.Je,hamuwaamini Forbes walioudhihirisha utajiri wake?Kwani ulitaka agawie watu fedha kama ubwabwa wa harusini ili asionekane bahili?
Utajiri wake haufanani na uhalisia.

Kuna siku nilikwenda Kisarawe ana eneo heka 150 lakini Pori tupu.

Nliibahatika kuonana na mlinzi wa eneo lile akanipiga kizinga,,

Eti hali mbaya sn.

Dah!! [emoji23][emoji23][emoji23].

Eti mlinzi wa shmba wa tajiri top 10 Africa ananipigia kizinga.
 
Back
Top Bottom