Hivi Msukuma halisi huwa anatokea wapi?

Big up mkuu
 
Kwa uzoefu wangu bhanyantuzu ndo jamii ya wasukuma ambayo ina elements za ubaguzi.
 
Lakini kumbuka wanyantunzu ni mchanganyiko wa wasukuma na wanyiramba, ndio maana hata baadhi ya majina wanachangia, kama Mangu mnyantunzu oia Mangu mnyiramba.@Kungu Kayuki,
 
Tawala za wasukuma kabla na wakati wa ukoloni zilikuwa 52. Mwenyekiti wa machifu wa mwisho wa wasukuma hadi Tanganyika inapata uhuru aliitwa Mtemi Majebele wa Mwagala. Kabla ya huyo Mwenyekiti alikuwa Makwaya wa Busia. Hilo ndilo eneo amblo wakoloni waliliita Sukumaland. Kwa sasa eneo hilo ni mkoa wa Mwanza isipokuwa wilaya ya ukerewe, mkoa wote wa Simiyu, mkoa wa Shinyanga isipokuwa wilaya ya Kahama na mkoa wa Geita isipokuwa wilaya za Bukombe, Mbogwe na Chato.
 
Usipotoshe watu. Sengerema ilikuwa wilaya ya Geita hadi mwaka 1976 ilipofanywa nayo kuwa wilaya. Aidha, Geita ilianza kuwa wikaya mwaka 1950 kabla ya hapo Geita na sengerema zilikuwa wilaya ya Mwanza siyo kwimba kama unavyopotosha wasomaji.
Wasukuma original ile OG wanapatikana Kwimba, hii wilaya imezaa wilaya za Magu, Missungwi na Sengerema na imebaki kuubwa tuu. Huko ndiyo Wasukuma OG tunatokea.
 
Umeandika sahihi kabisa Nyanda subi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wyatt Mathewson, Ukiona wengi wapo against nawe jitahidi kusoma kipi kipya wanaweza kukuongezea mfano usichoelewa kuhusu ni kuwa Ethiopia haikukaliwa na jamii na hii inathibishwa na location yake ambapo magharibi kulikuwa na mchanganyiko wa wabantu & waarabu Masharik wasomalis kusini wabantu & Nilotes kaskazini waarabu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…