DOKEZO Hivi Msumi ipo Dar es Salaam kweli?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

nzalendo

JF-Expert Member
Joined
May 26, 2009
Posts
12,106
Reaction score
12,916
Msumi ni Kilometer chache sana kutoka stendi ya mabasi ya Magufuli.

Sasa cha ajabu ni kwamba Msumi ipo kama vile hata wakuu wa Mikoa waliopita hapo Dar na wasasa si ajabu hawajui iko upande gani wa mji, achilia mbali DC.

Mbunge wa Ubungo (labda atapeleka pua) kwa ajili ya kampeni, Sina hakika na Mkurugenzi na blah blah wengine, kutoa umeme.
  • Msumi hakuna barabara.
  • Msumi hakuna zahanati zingatia ni eneo lenye kaya zaidi ya laki moja, Ref.Google Map.
  • Msumi hakuna kituo cha Polisi
  • Msumi hakuna maji ya bomba lakini kuna ofisi za CCM kila baada ya kilometer chache.
Kma si ushirikina wa Wamakonde ni nini?

Msumi hakuna madaraja baada ya kuzolewa na mvua, zingatia madaraja yote yalijengwa kwa nguvu za wananchi.

Tukisema Msumi hakuna Zimamoto tutakuwa tumeungana na washirikina manake mji mzima zimamoto ni moja tu pale faya kwa ajili ya Kariakoo na Muhimbili, hili hakuna kiongozi mwenye uwezo wa kulizungumzia manake akili zao ziko kunako matumbo yao.

Haya tuendelee Msumi Shule ya Msingi ni moja na haitoshi zingatia idadi ya kaya, nilisikitika mvua inanyesha wamesongana kibarazani kisa wanasomeaga chini ya mti.

Kuna majengo ya madarasa yapo upande wa kulia kama unaelekea msumi maeneo ya uwanjani sijui ni ya sekondari au ya msingi wenyeji mtatujuza.

Msumi hakuna kituo cha daladala ingawa daladala zipo kwa uchache zingatia hakuna barabara ndio kisa na wenye mabasi hawaitaki njia hiyo na abiria ni wengi sana sana kaya laki moja, mara waseme darajani mara waseme center lakini kote ni ushirikina tu.

Msumi hakuna miundo mbinu ya kukusanya taka.i.e Dampo kwa sasa hawataona athari.

Ngoja kidogo, kaya laki moja na kila siku watu wanazidi kuhamia, watu wa msumi hebu wekeni kero zenu hapa manake hampo jijini wala mamkoa.

Msumi Chui ametoroka msituni anaonekana mtaani, zingatia Msitu ameshapewa mwekezaji.

Pia soma: Dar: Shilingi bilioni 18 zatengwa kwa ajili ya kuimarisha upatikanaji wa maji safi Msumi iliyopo kata ya Mbezi
 
Mbona ujasema wamejenga wenye vipato, msumi hakuna shule wazazi wanapeleka shule watoto na magari yao, msumi hakuna maji watu wamechimba visima vyao, msumi hakuna zahanaati kwa sababu wakazi wa uko wana vipato vyao siyo issue kwenda hospital
Huko watu wamejenga vululuvululu
Maendeleo yatakujaje

Ova
 
Ni jimbo la Kibamba lote, mawasiliano ya barabara ni mtihani mkubwa sana, kipindi hiki watu wanaacha magari yao nyumbani, njia hazipitiki, wengine tupo 2.5km away from makao makuu ya wilaya ila network ya barabara utadhani tupo mashamba ya mpunga huko.

Futseke zao!
 
Karibia na uchaguzi mtapitishiwa grader lichonge barabara na kuweka kifusi. Halafu ataletwa mkandarasi wa barabara na kutangaziwa kuwa bajeti imeshatenga na upembuzi yakinifu unaendelea kwa mkandarasi kuwa site. Then uchaguzi ukipita tabu ileile. Mfano mzuri ni hiyo barabara yenu ya Mbezi Makabe kuna sanaa nyingi zimekuwa zikifanyika mwaka wa 7 huu sasa, mara kajengwe kalami mita 10 tena kanaanzia katikati ya barabara. Badala lami ianzie pale ilipo barabara ya goba , wao wamejenga kakipande katikati ambapo mwanzo na mwisho ni vumbi tu.

NINA KIWANJA HUKO MAKABE MSAKUZI KILA NINAPOPITA kwenye ile barabara nakata tamaa kabisa
 
Msumi ni Kilometer chache sana kutoka stendi ya mabasi ya Magufuli.

Sasa cha ajabu ni kwamba Msumi ipo kama vile hata wakuu wa Mikoa waliopita hapo Dar na wasasa si ajabu hawajui iko upande gani wa mji, achilia mbali DC.

Mbunge wa Ubungo (labda atapeleka pua ) kwa ajili ya kampeni, Sina hakika na Mkurugenzi na blah blah wengine, kutoa umeme
Msumi hakuna barabara
Msumi hakuna zahanati zingatia ni eneo lenye kaya zaidi ya laki moja Ref.Google Map

Msumi hakuna kituo cha Polisi

Msumi hakuna maji ya bomba lakini kuna ofisi za CCM kila baada ya kilometer chache.

Kma si ushirikina wa Wamakonde ni nini?

Msumi hakuna madaraja baada ya kuzolewa na mvua, zingatia madaraja yote yalijengwa kwa nguvu za wananchi.

Tukisema Msumi hakuna Zimamoto tutakuwa tumeungana na washirikina manake mji mzima zimamoto ni moja tu pale faya kwa ajili ya Kariakoo na Muhimbili, hili hakuna kiongozi mwenye uwezo wa kulizungumzia manake akili zao ziko kunako matumbo yao.

Haya tuendelee Msumi Shule ya Msingi ni moja na haitoshi zingatia idadi ya kaya, nilisikitika mvua inanyesha wamesongana kibarazani kisa wanasomeaga chini ya mti.

Kuna majengo ya madarasa yapo upande wa kulia kama unaelekea msumi maeneo ya uwanjani sijui ni ya sekondari au ya msingi wenyeji mtatujuza.

Msumi hakuna kituo cha daladala ingawa daladala zipo kwa uchache zingatia hakuna barabara ndio kisa na wenye mabasi hawaitaki njia hiyo na abiria ni wengi sana sana kaya laki moja, mara waseme darajani mara waseme center lakini kote ni ushirikina tu.

Msumi hakuna miundo mbinu ya kukusanya taka.i.e Dampo kwa sasa hawataona athari.

Ngoja kidogo, kaya laki moja na kila siku watu wanazidi kuhamia,
watu wa msumi hebu wekeni kero zenu hapa manake hampo jijini wala mamkoa.

Msumi Chui ametoroka msituni anaonekana mtaani, zingatia Msitu ameshapewa mwekezaji.
Kama Mnaishi wanyonge tupu huko nyie msubirini Yesu tu
 
Karibia na uchaguzi mtapitishiwa grader lichonge barabara na kuweka kifusi. Halafu ataletwa mkandarasi wa barabara na kutangaziwa kuwa bajeti imeshatenga na upembuzi yakinifu unaendelea kwa mkandarasi kuwa site. Then uchaguzi ukipita tabu ileile. Mfano mzuri ni hiyo barabara yenu ya Mbezi Makabe kuna sanaa nyingi zimekuwa zikifanyika mwaka wa 7 huu sasa, mara kajengwe kalami mita 10 tena kanaanzia katikati ya barabara. Badala lami ianzie pale ilipo barabara ya goba , wao wamejenga kakipande katikati ambapo mwanzo na mwisho ni vumbi tu.

NINA KIWANJA HUKO MAKABE MSAKUZI KILA NINAPOPITA kwenye ile barabara nakata tamaa kabisa
Kuna barabara waliweka hadi kibao cha kuanza ujenzi, lile bango limeshaanguka tayari. Serikali imejaa uhuni sana.
 
Msumi ni Kibaha, Pwani.
Sio kweli! Hiko wilaya ya ubungo. Unapandia mbezi mwisho unavuka barabara ya morogoro Road unaelekea hukoo ndani kasikazini ya goba! Kule kule kumejazana wabongo wachovu bila shaka! Ukifika mbezi mwisho utawaonea huruma walivyojipanga foleni wakisubiri migari yao michovu kama vile mibasi iliyokataliwa michakavu ndo inaendaga msumi/misumi
 
Back
Top Bottom