DOKEZO Hivi Msumi ipo Dar es Salaam kweli?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Kuna barabara waliweka hadi kibao cha kuanza ujenzi, lile bango limeshaanguka tayari. Serikali imejaa uhuni sana.
Bajeti iliyojenga barabara ya kwa msuguli -malamba mawili ndio hiyo hiyo ilikua ifike mpaka kwembe,king'azi,kifuru hadi kisarawe,ila jiwe alipokufa tu ile bajeti na yenyewe ikaenda mifukoni mwa wajanja,jiwe alikua mtu sana sema vzr avidumu
 
Kitu ambachi sielewi why Temeke imefanikiwa kuwa na Lami vichochoroni. Ubungo Moja ya manispaa yenye ukwasi mkubwa imeshindwa wapi!?
Tmk ilijiwahi kipindi cha jiwe,kama utakumbuka siku anazindua magu bus terminal aliongelea ujenzi wa barabara za wilaya ya ubungo na majimbo yake ubungo na kibamba,baada ya pale akuonekana tena hadharani hadi umauti wake,hawa waliokuwepo sasa hivi hawana time na maendeleo ya wananchi
 
Sisi tulishawahi tumewekeza biashara zetu vzr. Na maji yapo tumepata kutoka tanki la Tegeta A. Mtoa huu uzi aache kukatisha watu tamaa yeye akajenge Sinza au Kinondoni atuachie Msumi yetu. Maana hata Goba miaka ya 2012 ilikuwa worse no maji no umeme no barabara. New Msumi is coming!
 
Waambie waelewe. Sehemu niliyowekeza mimi kuna maji kutoka Tegeta A. Upande uliobaki Maji yatafika na fomu walishajaza. Maendeleo yanakuja .
 
Uvumilivu ni nguzo ya Kila kitu
 
Mkuu samahani, nikitaka kufika huko napitia wapi ? Nipo serious nataka nikafanye ziara huko nipaone.
Stand ya daladala mbezi mwisho ...ulizia magari ya Msumi.
 
Braba

Ya Mpigi magohe itajengwa pia kwenye huo mradi ?!
Barabara ya mpiji magohe serikali inashughulika na kibamba mpiji magohe mpka iishe inajengwa kwa awamu. Mbezi mpiji magohe bado Sana maana kipande hiki kinahitaji fidia kubwa kwa wananchi katika kupanua barabara pia kipande hiki kinahitaji Madarajq zaidi ya matano hivyo inahitajika bajeti ya kutosha
 
Barabara ya kiwango cha lami soon inakuja tenda ya kumpata mkandarasi imeshatangazwa. Msumi kumenoga endeleeni kupanga kinondoni na sinza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…