DOKEZO Hivi Msumi ipo Dar es Salaam kweli?

DOKEZO Hivi Msumi ipo Dar es Salaam kweli?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Barabara ya mpiji magohe serikali inashughulika na kibamba mpiji magohe mpka iishe inajengwa kwa awamu. Mbezi mpiji magohe bado Sana maana kipande hiki kinahitaji fidia kubwa kwa wananchi katika kupanua barabara pia kipande hiki kinahitaji Madarajq zaidi ya matano hivyo inahitajika bajeti ya kutosha
Nani kakwambia ile barabara kuna watu wanahitaji fidia..,barabara ya Mpigi Magohe ina mawe yamewekwa toka zamani hata ukipita utayaona haina cha fidia wala nn..,sema kuna kitu hakipo sawa pale.
Jana waziri alikuja kukagua daraja la mto Mpiji, barabara ilichongwa usiku kucha na haijawa kuchongwa kwa haraka kiasi hicho.
Ile barabara kuna watu watakuwa na maslai nayo...angalau kipindi cha Magufuli ilikuwa inacho kidogo lakini kipindi hiki wala hawajisumbu..,wananchi wanapata tabu barabara mbovu usafiri mda mwingine mapaka 3,000.
 
Barabara ya mpiji magohe serikali inashughulika na kibamba mpiji magohe mpka iishe inajengwa kwa awamu. Mbezi mpiji magohe bado Sana maana kipande hiki kinahitaji fidia kubwa kwa wananchi katika kupanua barabara pia kipande hiki kinahitaji Madarajq zaidi ya matano hivyo inahitajika bajeti ya kutosha
Kabla ya kuja waziri magari yalikuwa yanapita Kibamba karibu wiki yote hii kwa jinsi barabara ilivyokuwa mbovu..,jana waziri amekuja ilichongwa usiku kucha.
 
Msumi ni Kilometer chache sana kutoka stendi ya mabasi ya Magufuli.

Sasa cha ajabu ni kwamba Msumi ipo kama vile hata wakuu wa Mikoa waliopita hapo Dar na wasasa si ajabu hawajui iko upande gani wa mji, achilia mbali DC.

Mbunge wa Ubungo (labda atapeleka pua) kwa ajili ya kampeni, Sina hakika na Mkurugenzi na blah blah wengine, kutoa umeme.
  • Msumi hakuna barabara.
  • Msumi hakuna zahanati zingatia ni eneo lenye kaya zaidi ya laki moja, Ref.Google Map.
  • Msumi hakuna kituo cha Polisi
  • Msumi hakuna maji ya bomba lakini kuna ofisi za CCM kila baada ya kilometer chache.
Kma si ushirikina wa Wamakonde ni nini?

Msumi hakuna madaraja baada ya kuzolewa na mvua, zingatia madaraja yote yalijengwa kwa nguvu za wananchi.

Tukisema Msumi hakuna Zimamoto tutakuwa tumeungana na washirikina manake mji mzima zimamoto ni moja tu pale faya kwa ajili ya Kariakoo na Muhimbili, hili hakuna kiongozi mwenye uwezo wa kulizungumzia manake akili zao ziko kunako matumbo yao.

Haya tuendelee Msumi Shule ya Msingi ni moja na haitoshi zingatia idadi ya kaya, nilisikitika mvua inanyesha wamesongana kibarazani kisa wanasomeaga chini ya mti.

Kuna majengo ya madarasa yapo upande wa kulia kama unaelekea msumi maeneo ya uwanjani sijui ni ya sekondari au ya msingi wenyeji mtatujuza.

Msumi hakuna kituo cha daladala ingawa daladala zipo kwa uchache zingatia hakuna barabara ndio kisa na wenye mabasi hawaitaki njia hiyo na abiria ni wengi sana sana kaya laki moja, mara waseme darajani mara waseme center lakini kote ni ushirikina tu.

Msumi hakuna miundo mbinu ya kukusanya taka.i.e Dampo kwa sasa hawataona athari.

Ngoja kidogo, kaya laki moja na kila siku watu wanazidi kuhamia, watu wa msumi hebu wekeni kero zenu hapa manake hampo jijini wala mamkoa.

Msumi Chui ametoroka msituni anaonekana mtaani, zingatia Msitu ameshapewa mwekezaji.
Halafu utakuta boya wa msumi,makabe na kerege anamcheka mtu wa Kakonko kigoma,ama namanyere katavi ama sikonge tabora
 
Karibia na uchaguzi mtapitishiwa grader lichonge barabara na kuweka kifusi. Halafu ataletwa mkandarasi wa barabara na kutangaziwa kuwa bajeti imeshatenga na upembuzi yakinifu unaendelea kwa mkandarasi kuwa site. Then uchaguzi ukipita tabu ileile. Mfano mzuri ni hiyo barabara yenu ya Mbezi Makabe kuna sanaa nyingi zimekuwa zikifanyika mwaka wa 7 huu sasa, mara kajengwe kalami mita 10 tena kanaanzia katikati ya barabara. Badala lami ianzie pale ilipo barabara ya goba , wao wamejenga kakipande katikati ambapo mwanzo na mwisho ni vumbi tu.

NINA KIWANJA HUKO MAKABE MSAKUZI KILA NINAPOPITA kwenye ile barabara nakata tamaa kabisa
Niuzie
 
Barabara ya kiwango cha lami soon inakuja tenda ya kumpata mkandarasi imeshatangazwa. Msumi kumenoga endeleeni kupanga kinondoni na sinza.
Ilisemekana barabara itaanza kujengwa mwezi wa 7 na kwamba fedha za ujenzi zimeshatengwa tayari.

Sasa ujenzi umefikia wapi mkuu, maana kama walianza ujenzi mwezi wa saba kwa sasa mwezi wa tisa, hivyo miezi miwili hii watakuwa mbali kidogo.
 
Kuna mradi wq DMDP phase two watajenga barabara ya msumi kilometa 9.08 . Ujenzi unaanza mwezi wa saba. Kipindi wanatangaza zabuni ili mkandarasi apatikane. Tembelea page ya mkuu wa mkoa you tube autakuta kafafanua barabara ambazo zitapitiwa lami
Ok mkuu, kama ujenzi ulianza mwezi wa saba kama walivyoahidi, sasa tupe mrejesho wa walipofikia kwa sasa toka walipoanza huo ujenzi mwezi wa saba.

Maana tumeshaingia mwezi wa tisa sasa, hivyo kama walianza mwezi wa saba nina imani sasa hivi watakuwa wameshajenga hata kilometre mbili, au tatu za barabara.
 
Ilisemekana barabara itaanza kujengwa mwezi wa 7 na kwamba fedha za ujenzi zimeshatengwa tayari.

Sasa ujenzi umefikia wapi mkuu, maana kama walianza ujenzi mwezi wa saba kwa sasa mwezi wa tisa, hivyo miezi miwili hii watakuwa mbali kidogo.
Lami tayari mbona dakika 0 tupo Posta. Uko wapi unauliza hayo maswali ukiwa wapi.
 
Back
Top Bottom