Hivi Mtoto kabla hajazaliwa hupataje haja tumboni?

amos eglan

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2015
Posts
310
Reaction score
463
Habari wanajukwaa kama tunavyofahamu mtoto pindi anapokuwa tumboni hupata chakula kupitia mama yake kile anachokula na kunywa lakini nilikuwa nataka kujua kwa sababu kila unachokula lazima ukitoe kupitia haja.

Sasa kwa watoto waliopo tumboni wanapata haja kama kawaida na hutolewa na Mama au vipi?
 
Placenta (ndio inaunganisha mtoto na mama) hii hufanya kazi ya kumpatia mtoto hewa/oxygen na virutubisho/nutrients kwa mtoto kutoka kwa mama. Na ndio inatoa uchafu kutoka kwa mtoto kupitia damu.

Vyote hivyo nilivyoelezea ni kwa njia ya damu kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto/kwa mtoto kwenda kwa mama.
 
Kichwa Kichafu amekujibu verma kwenye perpective moja wapo. Perspective ya pili ni kwamba, ili haja itokee, chakula lazima kiingie mdomoni na kusafiri kwenye alimentary canal.

Alimentary canal inaanzia kwenye mouth, inapita kwenye aesophagus, inakwenda kwenye tumbo, inakwenda kwenye utumbo mwembamba then yale makapi yanasafirishwa kwenye utumbo mpana ambapo maji maji hunyonywa kwenye eneo la colon ambalo liko karibu kabisa na anus. Anus ndio njia ya upande wa pili ambayo inatumika kutoa haja.

Sasa kama chakula hakijaingia mdomoni, hakuna uwezekano wa mtoto kutoa haja akiwa ndani ya mfuko wa uzazi.
 
Nafikiri huwa wanajisaidia kwa njia ya mama mjamzito kutapika na lile tumbo kuwa kubwa ni kwa sababu ya zile haja yani ndogo na kubwa za mtoto kujaa sana kwa mama hivyo tumbo hujaa
 
Nafkiri huwa wanajisaidia kwa njia ya mama mjamzito kutapika na lile tumbo kuwa kubwa ni kwa sababu ya zile haja yani ndogo na kubwa za mtoto kujaa sana kwa mama hivyo tumbo hujaa
Duuuh! Sidhani kama ni hivyo. Kuna mdau hapo juu kajaribu kuelezea kiutaalamu akihusisha mfumo wa chakula unavyofanya kazi.
 
Nichumu Nibebike,
Kuna dada nilimpeleka kujifungua kwa njia ya KISU, daktari bingwa aliyefanya upasuaji akatuambia, mtoto alishajisaidia sana, tungechelewa ingeleta shida kubwa.

Bingwa huyu ndie aliyemzalisha binti huyo watoto wote watatu alionao kwa kisu.
 
Ni sawa
 
Nafkiri huwa wanajisaidia kwa njia ya mama mjamzito kutapika na lile tumbo kuwa kubwa ni kwa sababu ya zile haja yani ndogo na kubwa za mtoto kujaa sana kwa mama hivyo tumbo hujaa
Duu..! Wee kweli kilaza.
 
Kuna dada nilimpeleka kujifungua kwa njia ya KISU, daktari bingwa aliyefanya upasuaji akatuambia, mtoto alishajisaidia sana, tungechelewa ingeleta shida kubwa.

Bingwa huyu ndie aliyemzalisha binti huyo watoto wote watatu alionao kwa kisu.
These are unusual cases.
 
Nichumu Nibebike,
Asante kwa maelezo mazuri, nami pia niongezee juu ya haya.

In late pregnancy, mtoto huanza kutumia ile amniotic fluid inayomzunguka kwa kuinywa taratibu sana, hivyo mpaka anafika hatua ya kuzaliwa kunakuwa na kinyesi kwenye lower almentary canal(gastrointestinal track).

Kama anazaliwa kwa kutanguliza kichwa mtoto hujisaidia mara baada ya kuzaliwa. Na kama ataanza kujisaidia kabla hajazaliwa(mama akiwa kwenye uchungu) hiyo inaitwa foetal distress(ingawa sio wote) maana yake mtoto anaanza kuonesha dalili za kuchoka.

Kwa habari ya mtoto anayetanguliza matako kwenye process ya kuzaliwa, huyo anajisaidia mapema sababu hubanwa sana kiuno na tumbo( ingawa sio wote).

NB: Maada (thread) hii ni pana ili kuijua kiundani (ufafanuzi) wasiliana na daktari wa wanawake.
 
Kuna dada nilimpeleka kujifungua kwa njia ya KISU, daktari bingwa aliyefanya upasuaji akatuambia, mtoto alishajisaidia sana, tungechelewa ingeleta shida kubwa.

Bingwa huyu ndie aliyemzalisha binti huyo watoto wote watatu alionao kwa kisu.
Maana yake mtoto alianza kuonesha dalili za kuchoka kabla ya kuzaliwa. Kuchoka hutokana na uchungu wa muda mrefu, kitovu(umbilical cord) kujizungushia shingoni mwa mtoto, na sababu nyingine nyingi( za kitaalamu).

NDIO MAANA MAMA MJAMZITO ANASHAURIWA AWAHI KITUO CHA KUTOLEA HUDUMA ZA AFYA MARA APATAPO UCHUNGU, ni pamoja na kufanyiwa monitoring mapema so as in case shida yoyote ikijitokeza aweze kusaidiwa(eidha yeye au mtoto)
 
Nafkiri huwa wanajisaidia kwa njia ya mama mjamzito kutapika na lile tumbo kuwa kubwa ni kwa sababu ya zile haja yani ndogo na kubwa za mtoto kujaa sana kwa mama hivyo tumbo hujaa

BANGE HAIJAWAHI KUMWACHA MTU SALAMA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…