Hivi Mtu Aliyesoma EGM Anaweza Akaja kusoma AGRICULTURE ENGENEERING SUA?

Hivi Mtu Aliyesoma EGM Anaweza Akaja kusoma AGRICULTURE ENGENEERING SUA?

Ndio anaweza kabisa wapo wengi sana wapo Sokoine university of agriculture walimaliza EGM
 
cha msingi uwe na principal ya Advanced Maths na Physics/ Chemistry/Geography.....so kwa EGM ni possible
 
Elimu imekuwa rahisi sana,engineering unasoma bila msingi wa Physics
 
Naomba msaada kwa anayejua kuhusu hlo wakuu.

Ndio anaweza kabisa wapo wengi sana wapo Sokoine university of agriculture walimaliza EGM

Anaweza wa egm sua wapo wengi tu

cha msingi uwe na principal ya Advanced Maths na Physics/ Chemistry/Geography.....so kwa EGM ni possible

hahaha, mkuu, Physics ya O Level inatosha kabisa!

Hizo ndo digrii za kipuuzi kabisa! Unawezaje kusoma engineering bila kuwa na advanced Physics!
O-level physics ni rubbish tu! Kama kuna mtu amesoma hiyo engineering bila kuwa na A-level physics asijidanganye kwamba ni kawaida na akajiita eti naye ni injinia. Huyo, hicho cheti ni leseni tu ya kuonyesha watu lakini lazima kiwango chake ni chini chini kuliko waalimu wake.

Kuna kozi zilikosa watu wakaanza kukumba tu bila mpangilio, ili chuo kiongeze mapatao.
 
Kiukweli mkuu kozi yoyote ikishakuwa titled engineering, lazima adv. Physcs ihusike. Ukitaka angalia hata vitabu vya tcu-guide book utagundua...sijui wanaosema inawezekana kama wana mifano hai au wana hisi tu.
 
sina imani sana kama physics ni LAZIMA ila ni muhimu, lakini je embu jiulize tunataka huo msingi ili iweje? na je wao (ambao hawana physics au hawa maths) wakifika chuoni hawasomi hiyo physics? je hawafaulu? na hao waliosoma phy je hawafeli? na walipokuwa wanachaguliwa walimu hawakuliona hili? ifikie sehemu tusijilimit kwenye historia kama hawakusoma na wakifika shule wanasoma na wanafanya vizuri kuanzia class mpaka field na makazini sizani kama kuna ubaya...

Unachanganya mambo mengi bila sababu na pia usirahisishe bila sababu. Kila kitu kinahitaji msingi, principles, siyo historia. Hapa unaingiza mambo ya kufaulu. Kufaulu ni jambo tofauti kabisa. Kama umepita chuoni lazima uelewe kwamba siyo kila wakati kuna uhusiano wa kufaulu na kuelewa. Kumbuka tunazungumzia mazingira ya chuoni. Sehemu ambapo hakuna baraza la mitihani.

Kama Chuo kimeamua kuingiza wasiyojua Physics au hesabu hakina sababu ya kutowafanya wafaulu. Tunachokisema hapa ni elimu ya engineering. Unawezaje kuisoma bila kusoma Physics! Kuna mtu akasema eti Physics ya o-level inatosha, hii ikanipa picha kwamba hajui hata tofauti ya O & A-levels. Nawe sasa unaanza kusema huko chuoni asome Physics, ipi ya A-level? yaani chuoni waanze kufundhisha maana ya gravitation constant, venturi principle, etc.

Elewa hivi, Physics ni science, engineering ni applied science hivyo unaposoma engineering you are applying science. Hakuna tena muda wa kuanza kujifunza principles za sayansi.

Umenifahamu?
 
Chuo ni Universal studies kama mtu amekidhi vigezo atapewa admission,then anapimwa kila mhula akishindwa kinachofuata kudisco.Mbona wapo CBG&EGM wanasoma Agric. and irrigation engineerings pale they do wonder.
 
Back
Top Bottom