Hivi mtu kama Steve Nyerere anaongelea masuala ya nchi kama nani?

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Unajua kwenye nchi hii kuna mambo yanachekesha na wakati huo huo ni kama yanadhalilisha sana.

Steve Nyerere, msanii wa vichekesho na bingwa wa kulia misibani, AMEPEWA NA NANI MAMLAKA YA KUISEMEA SERIKALI YA TANZANIA? Kwanini viongozi wa Tanzania wameamua kudhalilisha mamlaka tuliyowapa kwa kiasi hiki?




Kama yupo kiongozi wa nchi hii anayetaka kumtumia huyu jamaa ni vema akamtumia kwenye masuala yake binafsi au nyumbani kwake , huyu hajawahi kuchaguliwa na yeyote wala kuteuliwa na yeyote kwenye jambo lolote la Nchi hii.

Acheni kutudhalilisha.
 
Hilo bango halisemi popote kwamba anaongelea masuala ya nchi. Wewe umetoa wapi?

Anavunja sheria gani kuongelea masuala ya nchi yake? Huo ndo uhuru wa kuongea au sio.

Kama waandishi wanaona hana tija waache kwenda it's that simple.
 
Kwani katiba inamzuia kuyaongelea hayo mambo ya kitaifa?
 
Hilo bango halisemi popote kwamba anaongelea masuala ya nchi. Wewe umetoa wapi?

Kama waandishi wanaona hana tija waache kwenda it's that simple.
Nikajua umemsikia , kumbe hamna kitu !
 
Huyu ni musiba mpya, kwa kipato hana hata uwezo wa kukodi sehemu yoyote, Kuna watu wasiojulikana wapo nyuma yake
 
Mleta mda una akili za kichagadema,basi andamaneni
 
Kwam amezungumzia mambo gani hio asubuh?
 
Kama kawa wazee fursa aka machawa lazima ujiongeleshe ongelesha unaweza ukasikika, kuna watu uchawa unawafanya waishi mjini anafamilia huyo inahitaji kula.
 
Mkuu na wewe umeanza kuwa bingwa wa kuitafsiri katiba kama mwendazake ?
unaweza kuongea chochote ni kweli , lakini huwezi kujipa usemaji wa Taasisi , mimi naandika mengi sana humu jf , lakini yale yanayopaswa kufanywa na viongozi namwachia Mnyika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…