R-K-O
JF-Expert Member
- Jun 27, 2023
- 482
- 2,178
Aina hii ya watu ni kama wana sumaku ya mvuto, mtu yupo simple tu anavaa kawaida, sura ya kawaida, uchumi wa kawaida lakini watu wanampenda sana uwepo wake, kuongea nae, kuchati nae, kwenda kumsalimia, n.k.
Ni mtu ambae hata akiwa mgeni sehemu flani basi kesho yake kashazoeleka, akikaa sehemu kashakusanya kijiji, ni mtu ambae hata ajenge mbali na mji watu wapo tayari kuchoma mafuta na kulipia nauli wamfate, hata watu wale serious / wakimya hapa wanaongea mpaka mnabaki kushangaa.
Hiki ni kipaji au?