Shine
JF-Expert Member
- Feb 5, 2011
- 11,481
- 1,368
Mwanaume anatakiwa afike nyumbani muda wowote. Hakuna muda muafaka wa mwanaume kuja nyumbani.
Mkuu inategemea na mikakati wakiyokubalia baina yao wawili ktk ndoa
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mwanaume anatakiwa afike nyumbani muda wowote. Hakuna muda muafaka wa mwanaume kuja nyumbani.
Muda wa mwanaume kurudi home ni pale mke wake anaifanya home inavutia na inatamanisha kurudi home. full stop (na muda wa mke pia unategemea juhudi za mume wake)
sio vizuri kuchelewa nyumbani! mwanaume unatakiwa kuwahi saa kumi na moja asubuhi kabla watu hawajaamka! ukichelewa zaidi ya hapo kwa kweli si vizuri kwani majirani na watoto watakuwa wameamka
Nimesoma Igwe ni kizunguzungu tu.
Kusema kweli masuala ya ndoa yanahitaji HESHIMA tu na si kitu kingine. Bahati nzuri siku hizi kuna mawasiliano ya kutosha na hivyo mwenza wako kama kweli unamjali na una sababu iliyokuzuia mpaka muda fulani usifike nyumbani, basi bila shaka anaweza kujua mapema\...Ingawa wengine wanatumia mawasiliano haya vibaya.
Hakuna ulazima wa kupangiana muda wa kurudi nyumbani na mwenzako kama mnaaminiana na kuheshimiana katika ndoa yenu.
Nafikiri mpaka watu wanaamua kuishi pamoja, kama mume na mke, watakuwa wanajuana vizuri na hata kuamianiana pia.
Kwa hiyo hili suala la kupangiana muda wa kurudi nyumbani si dalili ya mapenzi ya dhati na mwenza wako.
Hii imetuliaMuda wa mwanaume kurudi home ni pale mke wake anaifanya home inavutia na inatamanisha kurudi home. full stop (na muda wa mke pia unategemea juhudi za mume wake)
Hujaona mwanaume anaamua kufungua duka ili asiwe anaenda ofisini? we ongeza tu bidii utajionea mambo. lolkwahiyo wanaweza kurudi hata kama kazi hazijaisha ili mradi panavutia?
Eh kweli wengine walizaliwa na bahati zao! Mwanaume mwingine akirudi saa Saba usiku unashukuru MUNGU maana ukimsema basi kesho anakuja alfajiri!!.Jana jirani yangu wamebwatizana na mkewe kisa jamaa karudi nyumbani saa Nne usiku wakati kawaida yake saa mbili huwa anakuwa sebuleni anaangalia TV.
Nikajiuliza kwani ni haki kwa mwanaume kupangiwa na mke wake muda wa kurudi nyumbani? Muda wa mwanaume kurudi nyumbani ni upi?
Ninachokumbuka babu yangu aliwahi kuniambia when i was under eighteen ni kwamba mwanaume hachelewi kwake, meaning kwamba any time unaingia.
Homu boyi kuna mutu imeiba password yako?Mimi napata wakati mgumu sana kujibu hili jambo maana sidhani kama kuna muda maalumu wakurudi nyumbani. Mimi nadhani muda wowote mwanaume akitoka ofisini arudi nyumbani na si mambo ya kupita sijui happy hours, sijui bar au club...hii tabia ni ya wapi lakini watanzania? Kama tunatoka kwenda kupata nyama choma au beer mbili tutoke na familia zetu baada ya kufika nyumbani kuongea na familia kuhusu siku ilivyokuwa ndo kuelekea sasa kwa kinywaji au mlo wa jioni na familia either mke na watoto au kama hakuna watoto na mkeo au mumeo baada ya hapo kurudi nyumbani na kupumzika kwa ajili ya siku inayofuata. Hii tabia ya kutoka kazini kukaa bar mpaka saa 6 au 7 ndo inatufanya tunakuwa maskini maana muda mwingi tunatumia kulewa na kuumwa hangover siku inayofuata. Halafu tunalalamika maisha magumu kila siku. Kwanini tusiwe tunaishi kwa mipango. Na badala ya kujisifia kwa kukaa bar au kukesha usiku kucha basi tujisifie kwa kufanya kazi na kutengeneza pesa nyingi. Tuseme mwanaume kufanya kazi masaa mangapi kwa siku, au mwanaume kipato kiasi gani kwa mwezi...? Tuwe na sifa kwa mambo ya maana. Mwanaume hasifiwi kula ila kazi...! TUBADILIKE
Kwa nini isiwe baada ya kazi? wewe kwa nini unapenda aje muda huo?Saa mbili mpaka saa nne usiku ikizidi hapo kuwe na sababu ya kueleweka sio ooh ikaenda ikarudi nilipata emergency oh
mnatakiwa muwe karibu na family zenu ,mjue maendeleo ya watoto wenu..kuna matatizo gani nyumbani sitegemei uingie home saa sita muanze kupeana update na wife wakati ni muda wa kulala
Hii ratiba ya kuingia saa tano au sita usiku unalala asubuhi kazini kurudi tena saa sita usiku ...aggggh habari za familia mtazijuaje?
angalia usije anguka,maake hivyo viatu vilivyo virefu na kizingu zungu tena ni hatari,..anyway unaweza leta hapa kijiweni kwangu nivirekebishe na kuving'arisha pia
Hujaona mwanaume anaamua kufungua duka ili asiwe anaenda ofisini? we ongeza tu bidii utajionea mambo. lol
mie wangu akitoka tu kazini,namuexpect nyumbani sitaki kulea watoto ambao hawamjui baba yao vyema,anayekuja saa nne usiku ni irrensponsible father.
Hivi bado unaendelea na hiyo kazi?? sasa kinachokufanya uchelewe kurudi nyumbani ni nini wakati hapo kijiweni hakuna hata kibanda zaidi ya kile cha kuwekea rangi za viatu? ha ha ha ha
BTW: rangi ya viatu kama vyangu hapo juu utakuwa nayo kweli?
Jana jirani yangu wamebwatizana na mkewe kisa jamaa karudi nyumbani saa Nne usiku wakati kawaida yake saa mbili huwa anakuwa sebuleni anaangalia TV.
Nikajiuliza kwani ni haki kwa mwanaume kupangiwa na mke wake muda wa kurudi nyumbani? Muda wa mwanaume kurudi nyumbani ni upi?
wewe wasema.inaonesha ndio zako wewe kurudi usiku huna lolote ubabe wa ki mfumo dume tu .Mwanaume hapangıwı muda wa kurudi home.