Hivi Mungu anapenda kelele?

Hivi Mungu anapenda kelele?

Nyuki Mdogo

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2021
Posts
4,134
Reaction score
10,644
Nimesoma uzi mmoja wa Tycoon mmoja hapa Jf, anadai utafiti wake wa miaka 22 unaonesha Mungu wa walokole ndio ana nguvu kuliko Mungu anaeabudiwa na Madhehebu mengine.

Nimejaribu kuchunguza Mifumo wanayoitumia walokole wengi 100% katika ibada zao, maombi kiujumla huwa zimejaa kelele nyingi sana (elewa maana ya kelele wala sijadhihaki mtu)

Imefikia hatua wasipokua na umeme basi ibada huwa inapoa sana makanisani mwao.

Je, Bila kelele nyingi MUNGU hawezi kuinuka na kutetea watu wake dhidi ya shetani?
 
Nimejaribu kuchunguza Mifumo wanayoitumia walokole wengi 100% katika ibada zao, maombi kiujumla huwa zimejaa KELELE nyingi sana (elewa maana ya KELELE wala sijadhihaki mtu)

Imefikia hatua wasipokua na UMEME basi ibada huwa inapoa sana MAKANISANI mwao.

Je, Bila KELELE nyingi MUNGU hawezi kuinuka na KUTETEA watu wake dhidi ya SHETANI?
Kwani we ni Mungu? Una uhakika gani Mungu ana mtazamo kama wako juu ya hizo unazoita kelele?

Je labda yeye haoni hicho unachoona wewe? Inawezekana kwako ni kelele kumbe kwake ni kawaida sana! Pengine kwake ni sauti ya chini kiasi hata hawasikii na anatamani hata waongeze sauti!

Zitakuwa kelele pale zinapokuwa si takatifu mbele zake! Kama ni za kinafiki hapo kweli ni kelele hata Kama wananena kimoyomoyo! Mawazo ya Mungu si sawa na mawazo ya mwanadamu! Wewe siyo Mungu, acha kumsemea Mungu!
 
Mkuu japo sio nguli sana wa haya mambo ila nna uhakika maandiko yameagiza utulivu wa Hali ya juu wakati wa maombi na ibada kwa ujumla hata tunaposali tunaagizwa jirani zetu wasisikie tukifunga ndio kabisaaa ni wewe na moyo wako utashangaa siku hizi inafikia mahala mpaka watu wanalazimishwa kujificha kula kisa Kuna watu wamefunga hii sio sawa na ni kinyume kabisa na maandiko itoshe kusema Mungu yupo na haitaji kabisa mbwembwe na unafiki wa mwanadamu.Namalaga unene
 
Umesema vema sana kuwa wewe si nguli wa mambo hayo ya kiroho! Kimsingi hayupo aliye nguli!

Kuna wakati ni ngumu kuelewa mambo ya kiroho! Yanaweza kuwa kinyume sana na uelewa wako wa kibinadamu! Upumbuvu wa Mungu una hekima! Fuata Roho Mtakatifu analokwambia! Siyo Tycoon anachosema! Wakati mwingine anaweza kusema USIUE na wakati mwingine yeye huyo huyo anaweza kukwambia UA! Atakapokwambia UA usiseme ni dhambi! Atakalokwambia, fanya! Kama ni kelele angewaambia!
 
Nimesoma uzi mmoja wa Tycoon mmoja hapa Jf, anadai utafiti wake wa miaka 22 unaonesha Mungu wa walokole ndio ana nguvu kuliko Mungu anaeabudiwa na Madhehebu mengine.

Nimejaribu kuchunguza Mifumo wanayoitumia walokole wengi 100% katika ibada zao, maombi kiujumla huwa zimejaa kelele nyingi sana (elewa maana ya kelele wala sijadhihaki mtu)

Imefikia hatua wasipokua na umeme basi ibada huwa inapoa sana makanisani mwao.

Je, Bila kelele nyingi MUNGU hawezi kuinuka na kutetea watu wake dhidi ya shetani?
Thread 'Sala, dua na maombezi ya kimya' Sala, dua na maombezi ya kimya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Imani inapiga kelele.

Mungu hapendi ukimya. Anapenda utaratibu.

Kuomba mpaka kulia machozi ni kawaida. Yesu aliomba na akalia machozi ya damu.

Ukipita maeneo, porini, kijiji, mtaa ambao una ukimya sana uliopitiliza na hakuna maendeleo ya watu na makazi jua kuna matatizo ya kiroho.
 
Nimesoma uzi mmoja wa Tycoon mmoja hapa Jf, anadai utafiti wake wa miaka 22 unaonesha Mungu wa walokole ndio ana nguvu kuliko Mungu anaeabudiwa na Madhehebu mengine.

Nimejaribu kuchunguza Mifumo wanayoitumia walokole wengi 100% katika ibada zao, maombi kiujumla huwa zimejaa kelele nyingi sana (elewa maana ya kelele wala sijadhihaki mtu)

Imefikia hatua wasipokua na umeme basi ibada huwa inapoa sana makanisani mwao.

Je, Bila kelele nyingi MUNGU hawezi kuinuka na kutetea watu wake dhidi ya shetani?
Mungu wa walokole kiziwi
 
Maombi yanatakiwa yawe na utulivu wa Hali ya juu, sidhani kama mungu anataka kupigiwa kelele na kupandishiwa sauti za juu kwa sababu yeye anasikia hata ukinena moyoni.
 
Nimesoma uzi mmoja wa Tycoon mmoja hapa Jf, anadai utafiti wake wa miaka 22 unaonesha Mungu wa walokole ndio ana nguvu kuliko Mungu anaeabudiwa na Madhehebu mengine.

Nimejaribu kuchunguza Mifumo wanayoitumia walokole wengi 100% katika ibada zao, maombi kiujumla huwa zimejaa kelele nyingi sana (elewa maana ya kelele wala sijadhihaki mtu)

Imefikia hatua wasipokua na umeme basi ibada huwa inapoa sana makanisani mwao.

Je, Bila kelele nyingi MUNGU hawezi kuinuka na kutetea watu wake dhidi ya shetani?

Mungu hahitaji kelele, anausoma hitaji, moyo, maombi yako.
 
Kwani we ni Mungu? Una uhakika gani Mungu ana mtazamo kama wako juu ya hizo unazoita kelele?

Je labda yeye haoni hicho unachoona wewe? Inawezekana kwako ni kelele kumbe kwake ni kawaida sana! Pengine kwake ni sauti ya chini kiasi hata hawasikii na anatamani hata waongeze sauti!

Zitakuwa kelele pale zinapokuwa si takatifu mbele zake! Kama ni za kinafiki hapo kweli ni kelele hata Kama wananena kimoyomoyo! Mawazo ya Mungu si sawa na mawazo ya mwanadamu! Wewe siyo Mungu, acha kumsemea Mungu!
Twende pole pole mkuu. Ongea na reference ya maneno matakatifu.
Screenshot_20230806-110006.png

Hizo ni mistari zinazoonesha jinsi Mungu asivyotenganishwa na KELELE. Haijalishi ni za namna gani
 
Mungu anasikia hata ukiwaza tu moyoni

Mwanzo 18 : 12 - Kwa hiyo Sara akacheka moyoni mwake, akisema, Niwapo mkongwe, nitapata furaha, na bwana wangu mzee?

Mwanzo 18 : 13 - Bwana akamwambia Ibrahimu, Mbona Sara amecheka akisema, Mimi kweli nitazaa mwana, nami ni mzee?
Mungu ukinong'ona anasikia

1 Samweli 1 : 13 - Basi Hana alikuwa akinena moyoni mwake; midomo yake tu ilionekana kama anena, sauti yake isisikiwe; kwa hiyo huyo Eli alimdhania kuwa amelewa.

Lakini hapo tunaposali na kuomba kwa sauti kubwa huwa sipaelewi.
 
Mt 6:7 SUV

Nanyi mkiwa katika kusali, msipayuke-payuke, kama watu wa mataifa; maana wao hudhani ya kuwa watasikiwa kwa sababu ya maneno yao kuwa mengi.

Kuna watu huwa hadi wanajirusha wanaongea lugha hazieleweki. Mje mtuambie mnafanya hivi kwa mwongozo upi
 
Back
Top Bottom