hivi mwakinyo yuko right?

fimboyaasali

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2011
Posts
8,617
Reaction score
8,244
kama kuna mtu anajua vizuri hili suala hebu tuandikie hapa tujue mkweli nani,kati ya mwakinyo na promota,maneno yamekuwa mengi
 
kama kuna mtu anajua vizuri hili suala hebu tuandikie hapa tujue mkweli nani,kati ya mwakinyo na promota,maneno yamekuwa mengi
π™½πš’πš–πšŽπš˜πš—πšŠ πšŠπš•πš’πš’πšŽπš”πšžπš πšŠ πš”πš˜πšŒπš‘πšŠ πš πšŠπš”πšŽ πš™πš’πšŠ πš—πš’ πš”πšŠπš”πšŠ πšŠπš”πšŽ 𝚠𝚊 πšπšŠπš–πšž πšŠπš—πšŠπš–πš”πš˜πšœπš˜πšŠ πš–πš πšŠπš”πš’πš—πš’πš˜ πš—πšŠ πšŠπš—πšŠπš‘πš’πšœπš’ πš‘πš’πš’ πš’πš—πšŠπš πšŽπš£πšŠ πš”πšžπš–πš™πš˜πšπšŽπš£πšŠ
 
Mwakinyo ni mjanja mjanja japo sijui sakata linaendaje.
 
kama kuna mtu anajua vizuri hili suala hebu tuandikie hapa tujue mkweli nani,kati ya mwakinyo na promota,maneno yamekuwa mengi
mwakinyo kinachomsumbua ni ushamba, kukosa shule, upwani na kujifanya kama ameshafika. nadhani anahitaji meneja mzuri. kwenye kutafuta maisha kuna wakati unatakiwa kujifanya mjinga hata kama wanakupunja pesa so long as unaendeleza kukuza jina/kujiuza, kuna siku tu utapata mikataba mikubwa. kwa kile alichofanya jana na kile alichotuuzia mbuzi kwenye gunia Uingereza, amezidi kupoteza mashabiki sana. wenzake siku hizi hata asipopata pesa physically, umaarufu unakuwa mtaji mkubwa sana na kutunza mashabiki.
 
Anasema hana mkataba wa maandishi, kwa level yake kama kweli ameingia mkataba wa maneno tu hivyo, inashangaza.
cha kujiuliza, hao aliowabwaga, hata kama siku nyingine watakuja kuwa na mkataba mnono, watamwita? watu wametangaza shidano azam kwa kitambo, gharama kubwa afu yeye analeta mizaha?
 
kama kuna mtu anajua vizuri hili suala hebu tuandikie hapa tujue mkweli nani,kati ya mwakinyo na promota,maneno yamekuwa mengi
BONDIA Mtanzania Hassan MWAKINYO amethibitisha kuwa hakutakuwa na pambano lake dhidi ya Bondia kutoka Namibia, Julius Munyelele Indongo na kusitisha biashara ya ununuzi wa tiketi kwa ajili ya pambano lake hilo.

Aidha Mwakinyo ametoa ombi kwa Baraza la michezo Tanzania (BMT) kusimamia haki za Bondia Munyelele ambaye tayari yupo Nchini kwa ajili ya pambano hilo kwa mujibu wa sheria.

β€œFight has been cancel baada ya mazungumzo kuto fika atamu na sasa ni rasmi hakutakua na pigano langu hakuna tena biashara ya kununua ticket ...

β€œOmbi kwa wizara ya michezo na BMT naomba wasimamie haki za bondia Julius Indongo amefika kwa ajili ya pambano na sheria ni kama pambano limevunjika kwa bondia mmoja inabidi mgeni alipwe haki zake kwakua yeye amefika.

β€œNaomba simamieni promoter amemkana anasema hamjui na haya mambo hayana mwenyewe na sisi huwa tunasifiri kwenda nchi za watu yanaweza tukuta pia i hope litafanyiwa kazi.!! Next time!! Wanasema kufa kwa Imamu sio mwisho wa swala...” ameandika Mwakinyo kupitia ukurasa wake wa mitandao ya kijamii.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mapromota ni wahuni wahuni

Una mkanaje bondia?

Wao wanacho jali ni faida sio hasara

Makubaliano ya maneno pia ni sehemu ya mkataba endapo kuna mashahidi! Mwenye haki apate haki yake

Kama ni mgeni, promota au mwakinyo ila promota kumkana bondia ni tatizo kubwa, ana nikumbusha enzi za promota Msangi na vurugu zake
 
Wanamichezo wameanza kujitambua sasa,, wametajirisha sana watu kwa miaka mingi na kuachwa bila kitu baadae maisha yakianza kuwatandika ama wakiugua wanaishia kutembeza bakuli,, safi sana Mwakinyo safi sana Feisal Salum taratibu heshima itapatikana tu,,
 
sasa akipandishwa mahakamani ndio kazi sasa
 
Hizi siasa zenu leteni kwenye michezo migine sio ngumi.
Hivi unajua ukiongelea ngumi ni unaweka uhai wako rehani? Wewe hapo unaweza kuvumilia ngumi ya jicho hata Moja??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…