Hivi Mwanaume unakuwaje mtu unayeshinda umelala tu!?

Ni maneno kuntu kweli na haujayaumauma wakati ukighani!

Je risala hii uliyotoa, ina tofauti gani na mtu anayesema maneno haba yanayoonekana ni kejeli ya kuchochea ghadhabu za watu kwa kusema: "tafuta hela', bila ya muongozo wowote wala mbinu za fursa?

Umejitahidi kuelekeza kazi za kufanya katika kujitafutia riziki, kuna vijana ni wahitaji, lakini wamekwama kupata fursa hizo na wanahitaji kuelekezwa ili kukwamuliwa.

Je haujawahi kusikia mfumo wa mkwamo unavyofanya kazi: 'unauza kitu na haupati mteja' na mwingine 'anatafuta kitu hicho hicho unachokiuza wewe lakini hapati anayekiuza'?

Katika hali ya namna hiyo lazima kuwe na kiunganishi ambacho hukutanisha watu na kutoa fursa za watu kupata habari za fursa mbalimbali za kujipatia kipato.

Je kwetu hali ipoje?

Je ni kweli kuna vijana wamebweteka kiasi cha kufaria kupata 'ugali wa shikamoo' kama wao wanavyosema?

Nadhani tusiwalaumu moja kwa moja vijana, ni suala mtambuka, ni gonjwa la kijamii hili.
Mkuu umeongea pointi nzito sana na yenye ukweli 100%. Huo mkwamo wa muuzaji kukosa mteja na mhitaji kukosa muuzaji ndio changamoto kubwa ya kiuchumi tuliyonayo sasa hivi.

Ni kweli kabisa, neno tafuta hela pekee halitoshi bila kuonyesha mbinu. Na kiunganishi ulichokisema ndio kila kitu iwe ni kupitia mitandao, kuwaunganisha watu (brokerage), au kutengeneza majukwaa ya habari za fursa.

Je, kwa uzoefu wako au wa wadau wengine humu ndani, mnaona ni sekta gani au mifumo gani ambayo vijana wakijikita nayo inaweza kufanya kazi vizuri kama hicho 'kiunganishi' cha kukutanisha fursa na wahitaji
 
Hivi Mwanaume Unakuwaje Boya Unayeshinda Umelala

Wakuu, kuna muda inabidi tuongee lugha ya machinjioni kwa sababu hawa viumbe wanaojiita wanaume wa kizazi hiki wamezvywa mno na umama.

Inakuwaje mwanaume mzima, una ndevu kidevuni, una sauti ya besi kama honi ya lori la mkaa lakini huna fani yoyote, huna kazi, na huna hata mia mbili ya dharura mfukoni mwako
Upo upo tu mjini kama tambala la deki lililotelekezwa chooni.

Kazi yako kubwa ni kushinda umejilaza kitandani, unakodoa macho kwenye screen ya simu huku ukiwaza shemeji yako au dada yako atakurushia saangapi buku mbili ya kula ugali.
Hivi wewe ni mwanaume kweli au ni demu aliyesahau kuvaa sketi

Inakuwaje mwanaume unafikisha miaka 30 lakini mikono yako haina ujuzi hata mmoja wa kueleweka Hujui ufundi wa pikipiki, hujui kompyuta, hujui kushona, hujui hata kushika jembe ukalime vishamba vya pembezoni mwa mji.

Umekaa tu kizembe umepishana mikono kifuani kama binti aliyekataliwa ukweni.

Nikuambie ukweli unaoukwepa, Huu ujinga wa kushinda unajipaka mafuta mwilini, unanyoa viduku vya ajabuajabu na kuvaa pensi fupi mtaani ukiwa huna mia mbili, haukufanyi uwe mjanja. Unajiona handsome boy wa mjini

Siku shemeji yako akichoka kukulisha ugali, atakufungia mlango mchana kweupe na utarudi kwenu kijijini ukiwa umeshika nguo mbili kwenye mfuko wa sandarusi.

Amka wewe Futa hayo makamasi ya usingizi uelewe jambo moja, Dunia haijawahi na haitawahi kumhurumia mwanaume, Ukiona unatafuta huruma na dezo kama dada yako, jiandae kisaikolojia kulipia gharama yake kwa dharau kubwa zaidi Mjini hapa hakuna mtu atakayekulisha bure bila kukutumia kama tambala la deki

Usipojiongeza sasa hivi ukaingia barabarani kutafuta fani na hela yako mwenyewe, hawa watu unaowaomba mteremko watakufanya vitu ambavyo vitakufanya ujute kwanini ulizaliwa mwanaume

Kama huna fani wala kazi lakini unataka kuvaa nguo za gharama, kumiliki simu kali na kunywa bia, mjini kuna wazee ambao wanasubiri wavulana wapenda dezo kama wewe

Mwisho
Lakini nakuahidi, kitakachokupata mbeleni hakitahitaji mkalimani utakuwa mfano bora kwa wengine.
Mimi ofisi yangu ni nyumbani bana,akili kichwani,gari imepaki nje,ipo full tank,mchana napiga wali nazi na nguru au papa,hao waliopo busy kila wakati mlango ngo ngo ngo,tusevu bana ndani hakukaliki 😀😀😀!
-USIFANYE BIASHARA ZA UTULIVU KAMA WANGU UKIWA NA MIAKA 25-40,KWANI UMRI HUU NDIYO WA KUJENGA NJIA YA MAISHA YAKO!/KIMBIZANA SANA UMRI HUO.
 
Wote tukifanya kazi na kuwa na shughuli nani atamtuma mwenzake? lazima kuwe na watu ambao wanalala ili waamshwe watumwe kwenda kufanya vitu vya hapa na pale yaani wawe available 24/7.

Hao ni maalumu kutumwa vitu vya dharura sasa akiwa nje ya mji analima na imetokea dharura utamtuma nani?
 
Hivi Mwanaume Unakuwaje Boya Unayeshinda Umelala

Wakuu, kuna muda inabidi tuongee lugha ya machinjioni kwa sababu hawa viumbe wanaojiita wanaume wa kizazi hiki wamezvywa mno na umama.

Inakuwaje mwanaume mzima, una ndevu kidevuni, una sauti ya besi kama honi ya lori la mkaa lakini huna fani yoyote, huna kazi, na huna hata mia mbili ya dharura mfukoni mwako
Upo upo tu mjini kama tambala la deki lililotelekezwa chooni.

Kazi yako kubwa ni kushinda umejilaza kitandani, unakodoa macho kwenye screen ya simu huku ukiwaza shemeji yako au dada yako atakurushia saangapi buku mbili ya kula ugali.
Hivi wewe ni mwanaume kweli au ni demu aliyesahau kuvaa sketi

Inakuwaje mwanaume unafikisha miaka 30 lakini mikono yako haina ujuzi hata mmoja wa kueleweka Hujui ufundi wa pikipiki, hujui kompyuta, hujui kushona, hujui hata kushika jembe ukalime vishamba vya pembezoni mwa mji.

Umekaa tu kizembe umepishana mikono kifuani kama binti aliyekataliwa ukweni.

Nikuambie ukweli unaoukwepa, Huu ujinga wa kushinda unajipaka mafuta mwilini, unanyoa viduku vya ajabuajabu na kuvaa pensi fupi mtaani ukiwa huna mia mbili, haukufanyi uwe mjanja. Unajiona handsome boy wa mjini

Siku shemeji yako akichoka kukulisha ugali, atakufungia mlango mchana kweupe na utarudi kwenu kijijini ukiwa umeshika nguo mbili kwenye mfuko wa sandarusi.

Amka wewe Futa hayo makamasi ya usingizi uelewe jambo moja, Dunia haijawahi na haitawahi kumhurumia mwanaume, Ukiona unatafuta huruma na dezo kama dada yako, jiandae kisaikolojia kulipia gharama yake kwa dharau kubwa zaidi Mjini hapa hakuna mtu atakayekulisha bure bila kukutumia kama tambala la deki

Usipojiongeza sasa hivi ukaingia barabarani kutafuta fani na hela yako mwenyewe, hawa watu unaowaomba mteremko watakufanya vitu ambavyo vitakufanya ujute kwanini ulizaliwa mwanaume

Kama huna fani wala kazi lakini unataka kuvaa nguo za gharama, kumiliki simu kali na kunywa bia, mjini kuna wazee ambao wanasubiri wavulana wapenda dezo kama wewe

Mwisho
Lakini nakuahidi, kitakachokupata mbeleni hakitahitaji mkalimani utakuwa mfano bora kwa wengine.
Huu Uzi unaumiza macho, msiusome tafadhali.
 
Wote tukifanya kazi na kuwa na shughuli nani atamtuma mwenzake? lazima kuwe na watu ambao wanalala ili waamshwe watumwe kwenda kufanya vitu vya hapa na pale yaani wawe available 24/7.

Hao ni maalumu kutumwa vitu vya dharura sasa akiwa nje ya mji na imetokea dharura utamtuma nani?
[emoji3]
 
Mkuu vijisenti ulivyopata vilinde sana. Broke men are there Before Christ.

Duniani hapa usipende sana kutoa ushauri ambao hujaombwa. Some situations zipo ili nature ibalance maisha.
Mkuu umeongea ukweli mtupu. Hata Hao mashoga Kumbe nao pia ni part ya nature? Au vilaza au walala hoi
 
Mkuu umeongea pointi nzito sana na yenye ukweli 100%. Huo mkwamo wa muuzaji kukosa mteja na mhitaji kukosa muuzaji ndio changamoto kubwa ya kiuchumi tuliyonayo sasa hivi.

Ni kweli kabisa, neno tafuta hela pekee halitoshi bila kuonyesha mbinu. Na kiunganishi ulichokisema ndio kila kitu iwe ni kupitia mitandao, kuwaunganisha watu (brokerage), au kutengeneza majukwaa ya habari za fursa.

Je, kwa uzoefu wako au wa wadau wengine humu ndani, mnaona ni sekta gani au mifumo gani ambayo vijana wakijikita nayo inaweza kufanya kazi vizuri kama hicho 'kiunganishi' cha kukutanisha fursa na wahitaji
Good. Vijana ni nguvukazi, ni mali, katika taifa wanaitwa rasilimali watu.

Kwa mtu binafsi au uzoefu wa mtu mmoja ni vigumu sana kulitatua tatizo hili la ujobless wa vijana.

Isipokuwa kama taifa, Serikali inatakiwa iwaangalie vijana kama ni fursa ya nguvukazi isiyostahili kupotea bure katika ukuaji wake.

Kwa mfano 'Wizara ya vijana', ingeliweza kubuni fursa mbalimbali nje ya mifumo ya ajira rasmi ili kuwaboost vijana kujiajiri na kuwatafutia masoko ya bidhaa zao nk nk, mfano kuwakopesha nyezo za uzalishaji pamoja na mitaji bila riba.

Huu ni mfano mdogo nikitoa mwanga namna vijana wanavyoweza kusaidika, zipo fursa nyingi sana ambazo Serikali ikiamua kuwekeza katika vijana hakuna atakayekaa nyumbani bila kazi.

Kwa hali ilivyo sasa na kauli mbiu isiyo na fasiri ya 'vijana kujiari', haiwezi kufanya kazi yoyote kwa sababu, kujiajiri kunahitaji uwezeshwaji, lazima vijana washikwe mkono ndiyo waweze kutoka.
 
Back
Top Bottom