Hivi Mwanaume unakuwaje mtu unayeshinda umelala tu!?

Mkuu umeongea pointi nzito sana na yenye ukweli 100%. Huo mkwamo wa muuzaji kukosa mteja na mhitaji kukosa muuzaji ndio changamoto kubwa ya kiuchumi tuliyonayo sasa hivi.

Ni kweli kabisa, neno tafuta hela pekee halitoshi bila kuonyesha mbinu. Na kiunganishi ulichokisema ndio kila kitu iwe ni kupitia mitandao, kuwaunganisha watu (brokerage), au kutengeneza majukwaa ya habari za fursa.

Je, kwa uzoefu wako au wa wadau wengine humu ndani, mnaona ni sekta gani au mifumo gani ambayo vijana wakijikita nayo inaweza kufanya kazi vizuri kama hicho 'kiunganishi' cha kukutanisha fursa na wahitaji
 
Mimi ofisi yangu ni nyumbani bana,akili kichwani,gari imepaki nje,ipo full tank,mchana napiga wali nazi na nguru au papa,hao waliopo busy kila wakati mlango ngo ngo ngo,tusevu bana ndani hakukaliki 😀😀😀!
-USIFANYE BIASHARA ZA UTULIVU KAMA WANGU UKIWA NA MIAKA 25-40,KWANI UMRI HUU NDIYO WA KUJENGA NJIA YA MAISHA YAKO!/KIMBIZANA SANA UMRI HUO.
 
Wote tukifanya kazi na kuwa na shughuli nani atamtuma mwenzake? lazima kuwe na watu ambao wanalala ili waamshwe watumwe kwenda kufanya vitu vya hapa na pale yaani wawe available 24/7.

Hao ni maalumu kutumwa vitu vya dharura sasa akiwa nje ya mji analima na imetokea dharura utamtuma nani?
 
Huu Uzi unaumiza macho, msiusome tafadhali.
 
[emoji3]
 
Mkuu vijisenti ulivyopata vilinde sana. Broke men are there Before Christ.

Duniani hapa usipende sana kutoa ushauri ambao hujaombwa. Some situations zipo ili nature ibalance maisha.
Mkuu umeongea ukweli mtupu. Hata Hao mashoga Kumbe nao pia ni part ya nature? Au vilaza au walala hoi
 
Good. Vijana ni nguvukazi, ni mali, katika taifa wanaitwa rasilimali watu.

Kwa mtu binafsi au uzoefu wa mtu mmoja ni vigumu sana kulitatua tatizo hili la ujobless wa vijana.

Isipokuwa kama taifa, Serikali inatakiwa iwaangalie vijana kama ni fursa ya nguvukazi isiyostahili kupotea bure katika ukuaji wake.

Kwa mfano 'Wizara ya vijana', ingeliweza kubuni fursa mbalimbali nje ya mifumo ya ajira rasmi ili kuwaboost vijana kujiajiri na kuwatafutia masoko ya bidhaa zao nk nk, mfano kuwakopesha nyezo za uzalishaji pamoja na mitaji bila riba.

Huu ni mfano mdogo nikitoa mwanga namna vijana wanavyoweza kusaidika, zipo fursa nyingi sana ambazo Serikali ikiamua kuwekeza katika vijana hakuna atakayekaa nyumbani bila kazi.

Kwa hali ilivyo sasa na kauli mbiu isiyo na fasiri ya 'vijana kujiari', haiwezi kufanya kazi yoyote kwa sababu, kujiajiri kunahitaji uwezeshwaji, lazima vijana washikwe mkono ndiyo waweze kutoka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…