Hivi mwanaume unaweza kutenga siku kadhaa za likizo ukazitumia ukweni?

Hivi mwanaume unaweza kutenga siku kadhaa za likizo ukazitumia ukweni?

mzaza

Member
Joined
Mar 13, 2014
Posts
95
Reaction score
84
Habari zenu wanajamvi,

Ni miaka 8 sasa tangu nioane na mke wangu na tuna watoto watatu. Kwa ufupi tunaishi kwa amani sana. Tumejiwekea utaratibu kila mwisho wa mwaka huwa nachukua likizo na tunaenda na familia kijijini kwetu.

Mwaka huu amenikazia amesema inabidi twende nyumban kwao katika kipindi cha likizo(December). Kusema kweli familia yake(wakwe zangu) wako supportive sana na kusema kweli nawakubali. Binafsi napata kakigugumizi kumkubalia na kumkatalia wife.

Naombeni ushauri wenu ndugu zangu..
 
Kutoka kwa experience ya wazazi wangu tukiwa wadogo tulikuwa tunaenda likizo kijijini. Baba alioa kijiji kama cha tano hivi kutoka kijijini kwao. Hivyo likizo tulianzia kijijini kwa kina baba tunapiga kama wiki hivi halafu tunaenda kwa kina mama, baba anakaa kama siku 2 hivi anasepa anatuacha pale kwa kina mama kama two weeks hivi halafu anakuja anakaa 2 days tunanaondoka wote kwenda kijijini kwa baba tena na huko tunakaa kama 3 days then tunaanza safari ya kurudi nyumbani.

Hiyo ni experience ya ya utotoni. Mimi naishi Dar wazazi wa mke wangu asili yao ni Moshi, lakini wanakaa sinza. Kila baada ya mwezi tunaenda sinza kwa wazazi wa mke wangu tunakaa siku nzima tunarudi jioni.

Likizo mwezi wa december tunaenda vijijini. Tunapita kwao baba yake moshi kwao mama yake same kusamilia babu zake kama siku 3 then tunaenda kwa wazazi wangu maana baada kumaliza muda wao wa utumishi walendelea kukaa Arusha ambako mimi nimekulia. Tunapiga hapo kama wiki then tunaenda vijijijini kwa baba na mama ambako tunakaa siku 3 kila kijiji.

Kwa uzoefu hakuna ubaya. Ukwenu ni kwenu pia. Kama mazingira yanaruhusu unakaa tu kama siku kadhaa. Ila uwe na programme ya kufanya. Uzuri siku hizi hata vijiji vina guest house so unaweza kuwa unalala guest house.
 
Habari zenu wanajamvi,,
Ni miaka 8 sasa tangu nioane na mke wangu na tuna watoto watatu.,
Kwa ufupi tunaishi kwa amani sana.
Tumejiwekea utaratibu kila mwisho wa mwaka huwa nachukua likizo na tunaenda na familia kijijini kwetu.
Mwaka huu amenikazia amesema inabidi twende nyumban kwao katika kipindi cha likizo(December).
Kusema kweli familia yake(wakwe zangu) wako supportive sana na kusema kweli nawakubali.
Binafsi napata kakigugumizi kumkubalia na kumkatalia wife.

Naombeni ushauri wenu ndugu zangu..
Yeah, mi nilienda, nilirudi tako limeongezeka, ah eti tako, Kitambi. Maana nilikuwa nakula kuku tu hadi mama mkwe kuku wake wakaisha, ndipo nikaaga kuondoka.
 
Kutoka kwa experience ya wazazi wangu tukiwa wadogo tulikuwa tunaenda likizo kijijini. Baba alioa kijiji kama cha tano hivi kutoka kijijini kwao. Hivyo likizo tulianzia kijijini kwa kina baba tunapiga kama wiki hivi halafu tunaenda kwa kina mama, baba anakaa kama siku 2 hivi anasepa anatuacha pale kwa kina mama kama two weeks hivi halafu anakuja anakaa 2 days tunanaondoka wote kwenda kijijini kwa baba tena na huko tunakaa kama 3 days then tunaanza safari ya kurudi nyumbani.
Thnx
 
Nimependa hiyo ya kumaliza kuku wa mama mkwe .
Mama mkwe si alikuwa anajipendekeza, mimi nilikuwa sivungi, wakileta kabakuri kamejaa nyama namaliza zote halafu nakunywa na mchuzi..

Halafu kwenye stori mbili tatu na mama mkwe naanza kuchomekea, " kwa kweli mama mi napenda sana nyama ya kuku".

Niliwaacha hawana hamu na mimi, hadi leo waifu nikimwambia tukasalimie kwao anaanza kunichenga chenga...
 
KUSHINDA UKWENI NI INATEGEMEA ILA ITS BEST UNA WAACHA KIDS UNASEPA ZAKO ILA KUKAA ZAIDI YA😃SIKU KAZAA INAKUA MIYEYUSHO
 
Mm ukweni unilaz hata kwa usiku mmoja asee.. kuna mwamba alienda likizo ukweni kwake usku wamemilza kula wakasambaa kulala usku kabanwa mkojo ile kuamka na kuanza kupapasa ukuta labda soket iko hapa labda iko pale mara kapamia meza ya vyombo walivyolia chakula usku zle kelele za apa na pale na giza lile mama mkwe ikabid aamke ile kuwasha taa anamkuta mwamba maeneo ya daining si lkamtoka neno Baba kama ukushiba ungesema kulko hiki unachofanya mwamba kesho yake aliaga
 
[emoji3][emoji3][emoji3]
 
Back
Top Bottom