Hivi mwanaume unaweza kutenga siku kadhaa za likizo ukazitumia ukweni?

Hivi mwanaume unaweza kutenga siku kadhaa za likizo ukazitumia ukweni?

Mama mkwe si alikuwa anajipendekeza, mimi nilikuwa sivungi, wakileta kabakuri kamejaa nyama namaliza zote halafu nakunywa na mchuzi..

Halafu kwenye stori mbili tatu na mama mkwe naanza kuchomekea, " kwa kweli mama mi napenda sana nyama ya kuku".

Niliwaacha hawana hamu na mimi, hadi leo waifu nikimwambia tukasalimie kwao anaanza kunichenga chenga...
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Kutoka kwa experience ya wazazi wangu tukiwa wadogo tulikuwa tunaenda likizo kijijini. Baba alioa kijiji kama cha tano hivi kutoka kijijini kwao. Hivyo likizo tulianzia kijijini kwa kina baba tunapiga kama wiki hivi halafu tunaenda kwa kina mama, baba anakaa kama siku 2 hivi anasepa anatuacha pale kwa kina mama kama two weeks hivi halafu anakuja anakaa 2 days tunanaondoka wote kwenda kijijini kwa baba tena na huko tunakaa kama 3 days then tunaanza safari ya kurudi nyumbani.
haa. Ila uwe na programme ya kufanya. Uzuri siku hizi hata vijiji vina guest house so unaweza kuwa unalala guest house.
Uko vizuri sana
 
Sidhani kama kulala ukweni Kuna shida sema tu jamii zetu Zina ukakasi. Mie pia siwezi lala ukweni, kifupi sipendi hata kulala kwa ndugu. .

Uchagani ni mwiko kulala ukweni, kwanza nk matusi makubwa. Hata mke wangu haruhusiwi kulala kwao labda atokee mikoa ya mbali au Kuna shida kubwa mfano msiba na hata msiba kama ana uwezekano wa kurudi nyumbani anarudi. .
 
Mm ukweni unilaz hata kwa usiku mmoja asee.. kuna mwamba alienda likizo ukweni kwake usku wamemilza kula wakasambaa kulala usku kabanwa mkojo ile kuamka na kuanza kupapasa ukuta labda soket iko hapa labda iko pale mara kapamia meza ya vyombo walivyolia chakula usku zle kelele za apa na pale na giza lile mama mkwe ikabid aamke ile kuwasha taa anamkuta mwamba maeneo ya daining si lkamtoka neno Baba kama ukushiba ungesema kulko hiki unachofanya mwamba kesho yake aliaga
Nimecheka,, ni kama namuona jamaa anapigwa mkwara na mama mkwe vile..
 
Mama mkwe si alikuwa anajipendekeza, mimi nilikuwa sivungi, wakileta kabakuri kamejaa nyama namaliza zote halafu nakunywa na mchuzi..

Halafu kwenye stori mbili tatu na mama mkwe naanza kuchomekea, " kwa kweli mama mi napenda sana nyama ya kuku".

Niliwaacha hawana hamu na mimi, hadi leo waifu nikimwambia tukasalimie kwao anaanza kunichenga chenga...
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] aisee nimecheka balaa
 
Habari zenu wanajamvi,

Ni miaka 8 sasa tangu nioane na mke wangu na tuna watoto watatu. Kwa ufupi tunaishi kwa amani sana. Tumejiwekea utaratibu kila mwisho wa mwaka huwa nachukua likizo na tunaenda na familia kijijini kwetu.

Mwaka huu amenikazia amesema inabidi twende nyumban kwao katika kipindi cha likizo(December). Kusema kweli familia yake(wakwe zangu) wako supportive sana na kusema kweli nawakubali. Binafsi napata kakigugumizi kumkubalia na kumkatalia wife.

Naombeni ushauri wenu ndugu zangu..
Hakuna shida Mkuu,nenda ...N inaonekana Mungu amakujalia wakwe wema ...kama mazingira sio mazuri,unaweza kulala lodge ikibidi. Binafsi huwa naenda,nakula na mzigo kabisa...nakaa siku mbili tatu then nasepa,namwacha na watoto kwa muda mtakaokubalina kama familia...then unakuja kuwachukua...ofkoz huwezi kukaa mda mrefu ukweni,kunaboa unakua huna ishu...
 
Back
Top Bottom