Hivi mwenyekiti wa CCM huwa anajua anachokiongea?

Hivi mwenyekiti wa CCM huwa anajua anachokiongea?

Kwakua ni swali naweka kwa kifupi, CCM imechukua wanachama wengi wa Chadema na kuwapa uongozi wa juu serikalini, cha ajabu mwenyekiti huyo anayewapokea na kuwateua huku akiwaacha wananaccm wa siku nyingi anadai kuwa Chadema bado wachanga! Sasa hapa nani mchanga kati ya mwenyeji(CCM) na mgeni (Chadema)?
Ni lini kilaza akajua Ndugu yangu. Huyu ni kilaza kweli basi kadondokewq na embe chini ya mnazi
 
Kwakua ni swali naweka kwa kifupi, CCM imechukua wanachama wengi wa Chadema na kuwapa uongozi wa juu serikalini, cha ajabu mwenyekiti huyo anayewapokea na kuwateua huku akiwaacha wananaccm wa siku nyingi anadai kuwa Chadema bado wachanga! Sasa hapa nani mchanga kati ya mwenyeji(CCM) na mgeni (Chadema)?
Kwanza huwa unamwelewa?
 
Hamna kitu kichwani pale, tumepigwa kama Taifa!.
Eti juzi namsikia anawaambia TANAPA waruhusu madini kuchimbwa mbugani kwakuwa Simba na tembo hawayali madini yaliyomo ardhini!!.
Utetezi kama wa mtoto mdogo kabisa, anazijua vizuri hekaheka za migodi kweli huyu??. Si wanyama watahama wote kwa ma blasting.
Hata hivyo Serengeti imo kwenye orodha za urithi wa Dunia chini ya UNESCO, hawawezi ruhusu huo upuuzi!!.
Wengine hudhani madini yanapatikana kama vile tufanyavyo kwenda kwa sonara na kununua.
 
Mtoto mchanga ndiye Huwa anarubunika Kwa pipi, andazi, mdoli. Sasa hujaelewa nn hapo kuhusu kauli ya mama
 
Chadema kama taasisi bado ni wachanga, kama rufaa ya Msigwa imechukua muda mrefu hivyo, kama sio uchanga mi nini?

Kesi ya akina Mdee wameiendesha hovyo hovyo mpaka wanawafukuza. Chama kilochokomaa hakiwezi kufanya uonevu wa waziwazi tena kwa wanawake
Wachanga huku mnachukua viongozi wake na kuwapa vyeo.Loo! safari hii kazi pevu ukiona mpaka Msigwa kitumika lakini ngoma bado mbichi.
 
Back
Top Bottom