Hivi Mzee Baba huwa anasoma comments kule twitter baada ya kuandika tweets zake?

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Kwakweli ukipitia comments kila Mheshimiwa Sana anapo-tweet,unapata picha jinsi watu walivyo na machungu na hasira juu yake.

Swali ni je,Mheshimiwa Sana huwa anapitia hizo comments?

Na vijana wa Lumumba mbona hawajitokezi walau ku-balance equilibrium?

Kama anapitia, anajifunza mini?

Yaani asilimia zaidi ya 97 ni negative tu tena zenye lugha kali kabisa.

Mzee Baba, uje hivi ndivyo utakumbukwa maana jiulize watu hawa watasema nini siku ukitangulia mbele za haki kama leo uko hai ila comments ndio hizo?

Ushauri:Tumia kipindi hiki cha mwisho kujirekebisha japo huwezi ponyesha majeraha yaliyoko katika nafsi za watu ili walau upate mema machache ya kuongelewa vizuri.

Note:Unaesemwa vibaya zaidi ni wewe tu ila wanaokushangilia na kukusifu kwa kila jambo wao wala hawatajwi, na kama ni kutajwa, basi ni kidogo sana, hivyo ujue lawama zote utabeba peke yako.

Duniani tunapita jamani,tutende haki.
 
Hiyo account haendeshi yeye bwashee
Japo ni yake

Alafu Ukatae /Ukubali
Kuna watu Twitter wanafanya kazi kubwa ya kuwajaza ujinga vijana
Vitu vingine Uongo kabisa Lakini watu wanaretweet nakushadadia
Pita Instagram na Facebook bwashee kweny page za viongozi wako wa upinzani wanavyojibiwa uthibitishe nachosema
 
Jibu lako hili hapa

Credit to Next Man
 
Ashasema hashauriki na ukimshauri ndo unajaribu. Kwahiyo salary slip umeharibu
 
Mleta mada mbona unakuwa Kama siyo mkazi wa Tanzania bhana,
Tembelea akaunti za Yanga utakuta wanao comment wengi Ni watu wa Simba Tena kwa matusi na kejeri na matusi.

Tembelea akaunti za Simba utakuta Wana Yanga ndo wapo active ku comment Tena kwa matusi na kejeli.

Naomba kuishia hapo nafikri utakuwa umenielewa.
 
Jibu jingine murua ni hilo apo

Kwamba vinara wa kutukana na kukejeli ni wapinzani wa Magufuli na chama chake
 
Huwa najilazimisha tu huyu jamaa japo nimkubali lakini kiukweli huyu jamaa anayeitwa salary slip, daaah, ni moja la lijamaa bogas kabisa kuliko wote hapa Jf, limekaa kiumbea mbea tu,
 
Huo ni msimamo wako na wajinga wenzio
 
Huwa najilazimisha tu huyu jamaa japo nimkubali lakini kiukweli huyu jamaa anayeitwa salary slip, daaah, ni moja la lijamaa bogas kabisa kuliko wote hapa Jf, limekaa kiumbea mbea tu,
Tulia dawa iingie.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…