Hivi na huko majuu mechi za wenzetu huwa zinahairishwa kizembe zembe kama Derby yetu ya Kidwanzi ya Simba na Yanga?

Hivi na huko majuu mechi za wenzetu huwa zinahairishwa kizembe zembe kama Derby yetu ya Kidwanzi ya Simba na Yanga?

Tauceti Rigel

Member
Joined
Mar 6, 2025
Posts
5
Reaction score
9
Watu wamelipia tiketi za mabasi kutoka mikoani wengine wakiwa na go -and -return ila siku imeharibika

Kuna watu wamepika visheti na maudambu udambu kibao ambayo hayatakiwi kulala (usikute mtu kakopa OYA kabisa ili apige mpunga wa uhakika)

Vipi kwa wale ambao mechi za Simba na Yanga kwao ni kama stimu ya ngada? Alosto zao zimefikiriwa kwenye maamuzi haya?
 
Kukata tiketi na mechi kutochezwa huwa inatokea kwenye starehe yoyote ile, unaweza ukatuma nauli mwanamke asije.
Kikubwa gharama walishatumia hivyo hata ingechezwa hamna ambacho kingerudi
 
Tusubiri tarehe nyingine ya dabi itangazwe tu, kwa sasa tukubali matokeo kwamba 'Mabaunsa' Wametuheleleza.!

Sijui Walitumwa na nani ? Ikiwezekana alaaniwe aliyewatuma. Mabaunsa sio Watu kabisa.!
 
Hili jambo lililotokea lime ratibiwa na baadhi ya wanasiasa wenye ushawishi kwenye hizi timu... Unaweza ukajiuliza, inawezekana vipi mabaunsa wakawa na nguvu kiasi cha kuzuia timu isifanye mazoezi tena kwenye uwanja wa serikali?
Kuna muda nahisi TFF au TPBL hawako huru kufanya maamuzi muhimu ya kisoka kutokana na kuingiliwa na wanasiasa wenye nguvu na maslahi na hizi timu...
 
Mbele hakuna upumbavu kama huu, lazima kuwe na sababu yenye mashiko hasa kama hali ya hewa. Kutokuwepo Kwa usalama n.k lakini sio hizi sababu za kipumbavu za tff
 
Kumbe timu zina makomando wao, noma sana.
 
Majuu hakuna ujinga wa huku mazee kule unakata Tiket kwa seat yako kama haujafika kiwanjani hakuna mtu atakaa kwenye seat yako mpaka mpira unaisha maamuzi tunayotoa ya kiduanzi haya ya kina kasobho majuu walitoa miaka 60 iliyopita..
 
Hili jambo lililotokea lime ratibiwa na baadhi ya wanasiasa wenye ushawishi kwenye hizi timu... Unaweza ukajiuliza, inawezekana vipi mabaunsa wakawa na nguvu kiasi cha kuzuia timu isifanye mazoezi tena kwenye uwanja wa serikali?
Kuna muda nahisi TFF au TPBL hawako huru kufanya maamuzi muhimu ya kisoka kutokana na kuingiliwa na wanasiasa wenye nguvu na maslahi na hizi timu...
AFCON 2027 itakuwa ni aibu tupu. Mungu atupe uhai tu, utajionea mkuu..
 
Back
Top Bottom