Hivi na ninyi mna ndugu kama hawa?

Hahaha haaa huyo katisha zaidi maana hiyo ada lazima udai kweli
 
Yaani hii ni zaidi ya uchunguzi...mtu anahitaji kujua gharama ya maisha yako kiujumla
 
Ahahaa haaa utazani wanataka kukupunguzia gharama
Kuna nyumba nilisimamia ujenzi. Aisee watu wana mswali acha. Akipita anakuuliza hili ndo litakuwa jiko au choo? Ngazi fundi la kuharibia kaweka step kubwa sana....
 
Haya mambo yapo sana kwenye Familia zetu.
Mimi huwa nashusha thamani halisi (devalue) ili tu kuwaonyesha ni mambo tu madogo na yanawezekana.
Ninatoka kwenye Familia yenye watu wengi wa hali ya chini kimaisha na Mimi tu kwa kiasi kikubwa ndo nimefanikiwa hivyo ni nyota au star wa Familia kama sio ukoo, napata tabu sana kuwashawishi ili waone mambo nayoyafanya ni ya kawaida kabisa.
Juzi juzi nilinunua Prado inabidi nidanganye nimekopeshwa na Kampuni ili kuwaondoa Nyongo ni hatari sana mambo haya da.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…