Hivi na ninyi mna ndugu kama hawa?

Hivi na ninyi mna ndugu kama hawa?

Hahaha haaa huyo katisha zaidi maana hiyo ada lazima udai kweli
Kuna aliyekuwa anamsomesha mwanae English Medium. Shangazi yake alikuja kuugulia kwake pamoja na wasaidizi. Walimuuliza ada ya mtoto aliwajibu ni milioni 10 kwa mwaka.

Shangazi kusikia ile ada alitaka na nyumba yake ibadilishwe bati.

Alipata jibu la haraka kuwa kuna mzungu anamsomesha walikutana kanisani
 
Moja kati ya tabia huwa siipendi ni kuulizwa mshahara wangu, bei ya gari langu, pesa niliyotumia kujenga nyumba yangu. Huwa nazichukulia kama tabia za hovyo sana.

Halafu kuna ile tabia nyingine ya kuingia ndani na kuanza kukagua kagua vitu. Mara unataka uanze kupekua jokofu, mara unataka kukagua vyumba. Kuna wengine wakiona umepanga mavazi anaanza kujaribu na kung'ang'ania.

Tabia kama hizi ukizileta kwangu nakufukuza mchana kweupe. Usivuruge utaratibu niliowawekea watoto wangu.
Yaani hii ni zaidi ya uchunguzi...mtu anahitaji kujua gharama ya maisha yako kiujumla
 
Ahahaa haaa utazani wanataka kukupunguzia gharama
Kuna nyumba nilisimamia ujenzi. Aisee watu wana mswali acha. Akipita anakuuliza hili ndo litakuwa jiko au choo? Ngazi fundi la kuharibia kaweka step kubwa sana....
 
Haya mambo yapo sana kwenye Familia zetu.
Mimi huwa nashusha thamani halisi (devalue) ili tu kuwaonyesha ni mambo tu madogo na yanawezekana.
Ninatoka kwenye Familia yenye watu wengi wa hali ya chini kimaisha na Mimi tu kwa kiasi kikubwa ndo nimefanikiwa hivyo ni nyota au star wa Familia kama sio ukoo, napata tabu sana kuwashawishi ili waone mambo nayoyafanya ni ya kawaida kabisa.
Juzi juzi nilinunua Prado inabidi nidanganye nimekopeshwa na Kampuni ili kuwaondoa Nyongo ni hatari sana mambo haya da.
 
Back
Top Bottom