Hivi nani katuroga jamani.

Hivi nani katuroga jamani.

ndayilagije

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2016
Posts
7,491
Reaction score
8,304
Tumeambiwa sisi ni nchi ya top ten toka mwisho kwa furaha. Hilo halishangazi sana,kinachonishangaza ni hii tabia ya kushabikia vitu vya ajabu ajabu.Hivi tunategemea kupata furaha kwa kushabikia ujinga?
Yaani ukijua aibu ya mtu,au taabu na dhiki ya mtu tunaifurahia sana.
Tatizo liko wapi wenzangu,inakufaa nini kumcheka mtu,inakuongezea nini kusikia flani kafirisika, fulani kaachwa,au kafukuzwa kazi !!!
Unapata faida gani sasa!
Tutaendelea kukosa furaha mpaka kiama.
Mtu hata humjui sasa mateso au aibu zake wewe za nini?
Furaha tuwaachie wafini tu bwana maana wanajitambua.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mara nyingi wanaowacheka wengine ni wale walala hoi
Nisikubishie kwa kuwa umesema mara nyingi(siyo zote)lakini bado natatizwa na faida ninayoipata mchoma chipsi mimi kufurahia MD kufukuzwa kazi. Maana bado naiona future yake ya maana tu wakati mie nishapoteza mteja.Na hata kiimani mbona haipendezi!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom