Hivi naweza kununua kisimbuzi cha Azam tv Kenya na kuja kukitumia Tanzania?

Hivi watanzania ndio watu wakuvunwa? Kama kenya wanalipia Azam Pure 8,000 ya huku? Wakati sisi wana nzengo tunakamuliwa 18,000 ni haki kweli?
 
Mimi ni installer wa ving'amuzi vya satellite. Hata ukichukua kisimbuzi toka China, kinafanya kazi hapa Tanzania. Muhimu ujue frequency tu za kisimbuzi husika.

Hivyo inawezekena bila wasi.
 
kinapiga kazi mimi natumia dikoda ya Malawi inapiga kazi poa sana
Mkuu naomba unipe connection ya kupata cha Malawi, maana bei zao ndio poa kushinda hata cha kenya kwasasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…