Hivi naweza kuwa na UKIMWI kweli

Manselly

JF-Expert Member
Joined
Dec 17, 2010
Posts
456
Reaction score
130
Nambieni wadau,poleni na michakato ya katiba mpya na mvua hili duh ni noma(Niwaombe tu msikitumie hiki kipindi cha baridi na kushinda ndani vibaya itakula kwenu). Pamoja na maisha kuwa magumu bado jf inatupa raha kwa kutuunganisha watu kibao. Leo nina ka ishu kadogo jaman msinihukumu ila nipeni maoni yenu kwa hoja zifuatazo kama kweli naweza kuwa na ngoma?
1. Mara ya mwisho nimejihisi homa ni tar 2/3/2013 niliumwa kichwa nikanunua Phansidar mpaka leo na kumeza mpaka leo
2. Tangu nizaliwe sijawahi kulazwa wala kutundikiwa drip au kuongezewa damu wala mimi kutoa japo jamaa walikujaga shule wakafanya kampeni ya changia dam nikagoma.
3. Sijijali sana kwenye diet yani yaweza pita siku nzima kwa msosi mmoja au mara mbili tu kwa siku.
4. Nikinyoa ndevu au nywele zinaota fasta tu na zina afya pia nikijikata kidonda kinapona.
5. Ah nimekumbuka nilicheza game bila sox miaka miwili iliyopita lakini nimefatilia afya ya huyo dem mpaka leo mzma wa afya wala haumwi.
Nina umri wa miaka 27 na game zangu nyingi kwa sasa najitahidi kucheza safe.
Hebu nambieni wadau kwa mazingira hayo kweli bado naweza kuwa na ngoma?kweli mtu anaweza kunishawishi nikapime manake najiona kama sina sababu zaidi ya kuendelea ku play safe tu hebu nambieni wakuu wangu.
Nawasilisha
 
Umekuja kivingine..kwani kule umeambiwa vipi.. kapime bana..ata ukiwa na ukimwi hutakufa
 
Mkuu kwa dalili hizo kwa hakika una ngoma,nenda kapime ili ujue unaanza doze lini.
 
Usijiaminishe mia kwa mia, siku ukiambiwa pole ukimwi ni hali ya kawaidi cha muhimu jikubali tu kila kitu kitakuwa sawa na utaishi maisha marefu ya matumaini. Utajinyea ndugu.
 
Unaweza ukawa na ngoma hata kama hujaonekana na binti, nenda kapime.Safe nini! mitambo yenyewe feki pia misafe yako feki
 
ah wadau mbona mnanishutumu sana wakati mi nimeuliza tu kama kuna dalili au hali nyingine inayoweza kuwa kiashiria si tuambiane tu. Afu unavyoniambia nikapime ujue hiyo kauli hata ww inakuhusu
 
Unaweza ukawa na ngoma hata kama hujaonekana na binti, nenda kapime.Safe nini! mitambo yenyewe feki pia misafe yako feki

duh umetisha mkuu yani hadi mi safe yangu feki kweli we mkali inaonekana somo la kutofautisha FACTS na OPINIONS ulipata A
 
Ni hivi ukiambukizwa mfano leo huo ukimwi unaweza ukapima usionekane lkn baada ya miaka 5 ukaanza kuumwa yani vijidudu vinajitokeza sasa bora ukapime tu na tunashauriwa kujua afya zetu mara kwa mara sio mpaka upate sababu wewe ukikaa ukiona imepita miezi 3 au 6 cheki afya yako hata kama ni mara tatu kwa mwaka hapo utakuwa safe na ukizingatia kutochepuka na mwenzi wako .
 
Hivi unajua umezungukwa na watu wangapi walioathirika ila wamekula cobis tu wanachapa kazi? Kapime mshtuko ni mdogo halafu maisha yavaendelea.
 
eti 'nikijikata kidole kinapona!'......ekye kye kye kye!
 
acha uoga!! zingatia kanuni za afya njema, kula vitu vyenye faida mwilini mwako, acha pombe/vitu vitavyochosha viungo vya mwili wako unnecessarily,
 
mkuu UKIMWI haupimwi kwa macho!!

Nenda kapime afya yako uwe na uhakika!
 

yule jamaa wa saloon alikunyoa na wenzako mboma hujam taja hakusafisha na dawa alipomaliza kunyoya yule mwingine na wewe ukanyoa akakukata na mashine yenye damudamu
 
Mleta mada cna uhakika kama umemaliza hoja zko juu ya wacwac wko wa kuwa na huo ugonjwa.kunguru mwoga huficha ubawa wke.ila hongera kw kujilinda.
Kapime ukae kw amani.
 
Mkuu huo mda uliopoteza kuandaa hii Thread ungekuwa ushatoka Angaza na umeshaanza dozi maana inaelekea CD4 zako zimeshuka sana!
 
huo wasiwasi ndio utakaokufanya uanze kuugua.solution hapo ni moja tu nayo ni kupima.bila ya hivyo utaishi kwa wasiwasi siku zote.ila vielelezo vyako vimenichekesha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…