Hivi nchi za NATO hazina nguvu kabisa ya kijeshi?

kwisha

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2021
Posts
1,779
Reaction score
4,982
Vita si jambo la kushabikia sana, lakini nchi kama Urusi, Iran, Korea Kaskazini, na China zinaonekana kushabikia vita. Wanafikiri pengine ni wao pekee wenye nguvu kubwa za kijeshi na silaha za maangamizi, wakipeana sifa kiasi hicho.

Mara nyingi utasikia, "Korea itamshambulia Marekani," na unajikuta ukicheka.

Ninachoelewa ni kwamba nchi hizi zina nguvu kubwa sana, lakini zinaogopa kuanza vita moja kwa moja. Fursa hiyo imetumiwa na nchi kama Urusi na Korea Kaskazini kujipa kiburi.

Hata hivyo, wakiamua kuanzisha vita kamili, si rahisi kuwa mrusi au mkorea peke yake anaweza kupindua meza. Wote wanaweza kuangamia.

Nchi kama Uingereza na Ujerumani ni hatari sana pia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…