mwehu ndama
JF-Expert Member
- Nov 12, 2019
- 630
- 2,151
Wakati mashabiki wengi wa mwakarobo efusii au ukitaka waite mbumbumbu, wakisubiri kwa hamu mchezo wa Leo baina ya vidume Yanga afrika dhidi ya matapeli toka south Africa, kwa minajili ya kutafuta faraja baada ya wao kupakwa futa la nazi, na kisha kuliwa kiboga hapo jana. Mimi na timu Yangu ya kishushushu tayari tumeshalipata faili zima linaloonyesha mchezo utakavyokuwa na ni kwa namna gani timu ya taifa "Yanga Afrika" inakwenda kumvurumisha tapeli wa kizulu mamelod sundown pale Lupaso".
Kwanza ikumbukwe Yanga sc ni nchi ndani ya nchi, tunajeshi kubwa na ngome za kilozi kila pande ya Tanzania. Na nikatika nyakati za mechi dume kama hizi zinazofanyika hapa nyumbani ndipo ngome hizo huingia kazini bila woga wala huruma, na inaweza Kuwa bahati mbaya hata kwako wew shabiki wa Yanga ikiwa utaingia kwenye 18 za vigagula wetu katika maandalizi ya mchezo kama huu, sababu hawa wandewa wakiwa kazini kutetea Yanga afrika damu huwa zinamwagika maiti zinalazwa vyumbani mwa kubadilishia nguo kwa kifupi hii huwa ni vita kamili ya kiroho. Na mpaka muda huu Ninavyoandika uzi huu, tayari ngome zetu zote za kilozi zimekwisha rudisha mrejesho wa namna ramli zilivyoenda pale makao makuu na kwa bahati nzuri tayari kila chungu kimeonyesha Ubuntu botho wanakufa chuma si chini ya 2, na hii inatokana na wao pia kusafiri na kikundi cha wachawi 46 katika msafara wao toka south afrika wengi wakiwa na asili ya congo, la sivyo walikuwa wanakufa chuma si chini ya 5.
Ndani ya uwanja Leo yanga ataanza mchezo taratibu, pasi fupi fupi huku akimsoma mamelod ambaye yeye atakuja kwa pupa kutaka kupata goli la mapema ili arudi kulinda kisha kutuvizia kwa counter attack, lakini Yanga sc tutasimama imara bila kutetereka na mnamo dakika 37, pasipo kuelewa kilichotokea mamelod watashangaa mpira uko kunyavu na mfungaji akiwa ni maxi nzengeli. Wakati wakiwa katika mshangao huo, tukio kama hilo litajitokeza tena kipindi cha pili na safari hii itakuwa katika mazingira ya mpira wa kutenga ambapo mamelod watapigwa na bumbuwazi kisha kumuona mfungaji akifunga bila rapsha na wakati huu mfungaji atakuwa ni aziz ki dakika ya 77. Kosa watakalo lifanya mamelod second half wote tunalijua ila siwezi kulitaja, sababu hata wakati wanawasili Tanzania tayari walifanya mistake mbaya 2 ambazo hata uwe na timu ya namna gani, ukizifanya katika mechi ambayo yanga imeamua kutumia jeshi lake la kilozi huwezi toboa.
Viva Yanga Afrika