Hivi ndivyo Bahasha za Khaki zinavyodhalilisha vyombo vya habari vya Tanzania

mpaka magazeti yana muongozo na nyumba za ibada tunasubiria ilan ya CCM kabla kusema mungu tunasema samia mitano tena na mtoto wako kepenzi abdul.
 
Yaani vyombo Tofauti vimeelekezwa kuandika vile ambavyo mlipaji anataka.

Poor Tanzania!

View attachment 3354803View attachment 3354804
Is it coincidence au ni mpango mkakati...?

Inawezekanaje Mhariri wa gazeti la Nipashe na Mwananchi wawe na leading story yenye heading inayofanana neno kwa Neno...?

Hii taarifa imeandaliwa habari maelezo ya Samia Suluhu Hassan kisha wakatupiwa ili wachapishe hivyo hivyo...!

Kila mahali ni kutishwa tu...

Na tuvihurumie tu hivi vyombo vya habari na waandishi wao maana masikini hawa wakikataa kugoma kuchapa habari kinyume na matakwa ya "Fandungo state" chombo Chao cha habari au gazeti linafungiwa kama kanisa la Askofu Gwajima lilivyofungiwa bila hata ya notice...!!
 
Tanzania hakuna vyombo vya Habari.

Mwisho wa kuwa na vyombo vya Habari Tanzania ilikuwa mwaka 2015.
 
Hivi bado kuna watu wanahangaika na kusoma magazeti hadi sasa?

Tena magazeti yenyewe ya machawa matupu hakuna habari ambazo ni balanced badala yake zimeegemea upande mmoja tu wa kusifu na kuabudu kama tupo mbinguni.
 
Ukiwa kwenye sekta ya habari utawaelewa Hawa watu. Wenye vyombo vya habari mara nyingi wenyewe ndiyo huelekeza nini cha kuandikwa/kutangazwa,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…