PreGE2025 Hivi ndivyo CHADEMA yaweza kujinasua kwenye mtego wa kupasuka

PreGE2025 Hivi ndivyo CHADEMA yaweza kujinasua kwenye mtego wa kupasuka

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Elias Msuya

Platinum Member
Joined
Dec 23, 2011
Posts
267
Reaction score
1,014
WhatsApp Image 2025-04-06 at 18.15.46.jpeg

Ni wazi kwamba mambo si shwari ndani ya Chadema. Hiyo ni kutokana na kuibuka kwa kundi la G55 linalohusisha makada wa chama hicho wakipinga kampeni ya No Reforms No Election inayoendelea.

Kwa mujibu wa msemaji wa kundi hilo linalojiita la watia wa kugombea ubunge na udiwani, John Mrema amesema hawapingi kudai mabadiliko, lakini wanaona haiwezekani chama hicho kuzuia uchaguzi.

Kabla ya kuibuka kwa kundi hilo, kuna madai yaliyoibuliwa na Mwenyekiti wa Chadema wilayani Mwanga Mkoa wa Kilimanjaro, Lembrus Mchome akidai kuwa uteuzi wa viongozi wa chama hicho akiwamo Katibu Mkuu John Mnyika, Manaibu katibu wakuu (Bara na Zanzibnar) na baadhi ya wajumbe wa kamati kuu Januari 22, 2025 haukufuata Katiba na kanuni za chama hicho.

Ameshapeleka malalamiko yake hadi kwa Msajili wa vyama vya siasa akitaka aingilie suala hilo. Awali viongozi wa Chadema walimpuuza, lakini tangu alipoanza kumhusisha Msajili wa vyama Siasa sakata linaendelea kuchukua sura mpya.

Japo viongozi wa juu wa chama hicho, Mwenyekiti Tundu Lissu na John Heche wakiendelea na mikutano ya kampeni ya No Reforms No Election mikoa ya Kusini, wenzao wako Dar es Salaam wamekazana kuchokonoa chama hicho wakidai kuwa wanakisaidia chama chao kisife.

Kuna kila dalili kwamba chokochoko zote ni hizi ni maumivu ya kushindwa uchaguzi, hivyo sasa wanaoziibua wanatafuta namna ya kufurukuta ndani ya chama hicho ili waonekane kuwa nao wapo.

Hiyo ni kutoana na idadi kubwa ya wanachama wa G55 ni wale wale waliokuwa wakimuunga mkono Mwenyekiti aliyemaliza muda wake, Freeman Mbowe, ambaye alishindwa kutetea kiti chake cha uenyekiti.

Hatua hii inaupa mzigo mzito uongozi wa Lissu kwa chama hicho, kwani sasa anakabiliwa na maadui wakubwa wawili mbele yake, yaani adui wa kawaida ambaye ni CCM na sasa kuna adui wa ndani yaani wanachama wenzake.

Lissu akabilianaje na mgogoro huu?

Chadema itajikwamuaje?

Pamoja na ukweli kwamba Lissu na Heche walishinda uchaguzi huo, bado wakumbuke kwamba ushindi walioupata ni nusu ya walioshindwa. Katika uchaguzi huo, Lissu alipata asilimia 51.5 ya kura, huku Mbowe akipata asilimia 48.3 ya kura hizo.

Kwa hesabu hiyo inaonyesha waliokuwa wakimuunga mkono ni karibu nusu ya walioshinda. Sio kundi la kudharau na kulitenga. Ilitakiwa Lissu aanze kushughulika kwanza na kundi hilo kabla ya lolote katika ratiba hizo.

Wakati Mbowe anahutubia baada ya kushindwa uchaguzi katika ukumbi wa Mlimani City Januari 22, 2025, aliutaka uongozi mpya kuanza kutibu majeraha kwanza. Majeraha hayo sasa yanaonekana kusumbua.

Ilipaswa Lissu na viongozi wake watoe kipaumbele kwa kundi hilo ambalo japo limeshindwa linaendelea kuwa na machungu.

Wapo wanaosema kuwa Lissu ana uhalali kwa kuwa alishinda uchaguzi, ni sawa. Wapo wanaosema kuwa hata kampeni ya No reforms No election iliamuliwa kwenye vikao vya chama, hivyo ni kutekeleza tu. Ni sawa, lakini haya mambo ya kuyaendea kwa uangalifu sana.

Ndio maana nasema Lissu anapaswa kulingalia kundi hili kwa umakini mkubwa. Sio kuwabembeleza, hapana. Kinachopaswa kufanya ni kuketi vikao vya maridhiano kati ya uongozi na G55 kujadili ndani ili kumaliza tofauti zao.

Kuna taarifa kuwa baadhi ya wazee ndani ya chama hicho wameshaanza kutafuta suluhu kati ya Mbowe na Lissu. Hilo ni jambo jema, lakini juhudi Zaidi zinahitajika ili kuponya majeraha haya.
chadema-g55-pic-data.jpg


Tatizo la vyama vya upinzani ni kwamba, migogoro inapotokea, njia za utatuzi wake huwa zinakuwa ngumu, kwa sababu havina mamlaka ya Dola. Ingekuwa kwa CCM lingekluwa jambo rahisi tu. Kwa mfano, Mwenyekiti wa chama ambaye ndiye Rais wa Jamhuri ya Muungano, angetumia mamlaka yake tu ama kuwapa vyeo wanaolalamika au hata kuvitumia vyombo vya Dola kuwashughulikia wanaolalamika.

Utakuta huyu amepewa ukuu wa wilaya, mara mkuu wa mkoa, bara balozi nje ya nchi na vyeo vingine vingi.

Kwa CCM, hata Msajili wa vyama vya siasa ni mteule wa Rais ambaye pia ni mwenyekiti wa chama. Kwa hiyo hata kesi ikipelekwa kwa kwa mamlaka hiyo, hata Msajili mwenyewe ataiogopa. Lakini Kwa Chadema, kesi ikipelekwa kwa Msajili maana yake wamejichongea wenyewe.

Sasa kwa kuwa Chadema hawana mamloaka ya Kidola, njia wanazopaswa kuzitumia zinapaswa kuwa makini sana. Kwanza kuna uwezekano mkubwa wa CCM kuingilia kwenye migogoro hiyo na kuongeza ukubwa wa tatizo.

Hivyo, pamoja na ukweli kwamba Lissu na Heche waliwashinda wasijichukulie kwamba wao ndio kila kitu kwenye chama. Watoe nafasi na kwa kundi lililoshindwa. Ikiwezekana watoe vyeo na madaraka mbalimbali ndani ya chama hicho, ili kundi hilo lisijione kuwa limeachwa.

Ikiwa G55 wataendelea kutunisha misuli na uongozi wa chama nao ukatunisha misuli, kuna hatari kubwa ya chama hiki kusambaratika na kufuata mkondo ule wa NCCR Mageuzi na CUF. Hivyo kuna haja ya kuwa na hatua za haraka za usuluhishi.
 
Back
Top Bottom