Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Hii ni kwa Mujibu wa CAG
"Nilibaini kuwa Bohari Kuu ya Dawa ilinunua mashine 10 za kuondoa maumivu, ukakamavu na mkazo wa misuli (Diathermy) kwa bei ya shilingi milioni 136.7 na kuacha kununua vifaa hivi kwa mzabuni aliyebainika kuwa na bei ndogo wakati wa ushindani ya shilingi milioni 103.2 hivyo kupelekea gharama za ziada ambazo zingeweza kuepukika za kiasi cha shilingi milioni 33.5" -Kichere
"Vilevile nilibaini ununuzi wa vifaatiba kwa wazabuni 32 waliopewa zabuni zenye thamani ya shilingi bilioni 4.14 bila kufanyiwa uchambuzi wa awali na kuidhinishwa na bodi ya zabuni, pia vifaatiba vyenye thamani ya shilingi bilioni 13.37 ambavyo ununuzi wake haukuwa umeanza.
Pia nilibaini uchelewaji wa ununuzi na usambazaji wa vifaatiba katika vituo vya afya kwa siku zinazoanzia 23 hadi 1,458 tangu fedha zilipopokelewa na Bohari Kuu ya Dawa hadi vifaatiba vilipofika kwenye vituo vya afya, pia vituo 21 vya afya vilipokea vifaa vyenye thamani ya shilingi bilioni 1.68 ambavyo vilikuwa havijaanza kutumika" -Kichere
CAG Charles Kichere amezungumza hayo alipokutana na wanahabari Aprili 15.2024